250 – Muhammad bin ´Aliy bin Maymuun ametukhabarisha: Muusa bin Ayyuub ametukhabarisha: Makhlad bin Yaziyd ametukhabarisha, kutoka kwa Bashiyr, kutoka kwa Sayyaar, kutoka kwa Twaariq bin Shihaab, kutoka kwa Ibn Mas´uud, ambaye amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Watu hawazidishi chochote kwa dunia isipokuwa tamaa na dunia haiwazidishii chochote isipokuwa kuwafanya wawe mbali zaidi.”
251 – Ma´mar bin Sahl ametuhadithia: ´Ubaydullaah bin Tammaam ametukhabarisha, kutoka kwa Daawuud bin Abiy Hind, kutoka kwa Muhammad bin Siyriyn, kutoka kwa Abu Muusa, aliyesimulia:
“Mtu mmoja alikuja na kusema: “Ee Mtume wa Allaah! Mtu anapigana kwa ajili ya ushabiki, kwa ajili ya ujasiri na kwa ajili ya dunia.” Ndipo Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) akasema: “Yule mwenye kupigana ili neno la Allaah liweze kuwa juu, basi huyo ndiye yuko Peponi.”
252 – Muhammad bin Mansuur ametuhadithia: Aswad bin ´Aamir ametukhabarisha: Abu Bakr bin ´Ayyaash ametukhabarisha, kutoka kwa Sulaymaan at-Taymiy, kutoka kwa Anas, kutoka kwa Zuraarah, kutoka kwa Sa´d bin Hishaam, kutoka kwa ´Aaishah, kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), ambaye amesema:
“Nisingetaka kuwa na ulimwengu mzima kuliko Rak´ah mbili za kabla ya Fajr.”
253 – Abu Yuusuf Ahmad bin Muhammad ametuhadithia: Muhammad bin Salamah ametukhabarisha, kutoka kwa Abu ´Abdir-Rahiym, kutoka kwa Zayd bin Abiy Unaysah, kutoka kwa Wahb bin Kaysaan, kutoka kwa Ma´bad bin Ka´b bin Maalik, kutoka kwa Abu Qataadah, ambaye ameeleza:
“Tulikuwa tumekaa kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) wakati kulipopitishwa jeneza. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema: “Mmoja amepumzika na mwingine kumepumzishwa kutokana naye.” Tukasema: ”Ee Mtume wa Allaah, ni nani ambaye amepumzika na mwingine kumepumzishwa kutokana naye?” Akasema: “Muumini hufa, ambapo akapumzika kutokana na maradhi, uchovu na maudhiko ya dunia. Wakati huohuo kafiri wanapumzika kutokana naye waja, miji, wanyama na miti.”[1]
254 – ´Abbaas bin Muhammad ad-Dawriy ametukhabarisha: ´Ubaydullaah bin Muusa ametukhabarisha: Abul-´Anbas ametukhabarisha, nadhani kuwa, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Abu Hurayrah, ambaye amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Siku ya Qiyaamah kuna watu watakuja nyuso zao zikiwa hazina nyama; walizichosha kwa kuombaomba duniani.”[2]
255 – Abu Bakr bin Abiy ´Aaswim ametukhabarisha na amesimulia kutoka kwa Yahyaa bin Ishaaq: Ibn Lahiy´ah ametukhabarisha, kutoka kwa Abul-Aswad, kutoka kwa ´Urwah na al-Qaasim, kutoka kwa ´Aaishah, ambaye ameeleza:
“Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) alikuwa hapendezwi na chochote katika dunia. Wala hakuna kitu kilichompendeza kutoka humo isipokuwa iwe kumcha Allaah.”
256 – Abu Bakr bin Abiy Shaybah ametukhabarisha: ´Ubaydah bin Humayd ametukhabarisha, kutoka kwa ´Abdul-Malik, kutoka kwa Musw´ab bin Sa´d, kutoka kwa Sa´d, ambaye amesimulia:
“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) alikuwa akitufunza maneno haya:
اللَّهُمَّ إنِّي أَعُوذُ بكَ مِن فِتْنَةِ الدُّنْيَا، وعَذَابِ القَبْرِ
”Ee Allaah! Najilinda Kwako kutokana na mtihani wa dunia na adhabu ya ndani ya kaburi.”[3]
257 – al-Hasan bin ´Aliy ametukhabarisha: ´Abdus-Swamad ametukhabarisha, kutoka kwa Shu´bah, kutoka kwa ´Abdul-Malik bin ´Umayr, kutoka kwa Musw´ab bin Sa´d, kutoka kwa Sa´d, kutoka kwa Mtume (sallâ Allâhu ´alayhi wa sallam) mfano wa hayo.
258 – Abu Bakr ametukhabarisha: Husayn bin ´Aliy ametukhabarisha, kutoka kwa Zaa-idah, kutoka kwa ´Abdul-Malik, kutoka kwa Musw´ab bin Sa´d, kutoka kwa Sa´d, kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) mfano wa hayo.
[1] al-Bukhaariy (6512) na Muslim (950).
[2] al-Bukhaariy (1475) na Muslim (1040).
[3] al-Bukhaariy (6390).
- Muhusika: Imaam Abu Bakr Ahmad bin Abiy ´Aaswim ash-Shaybaaniy (a.f.k. 287)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Kitaab-uz-Zuhd, uk. 66-68
- Imechapishwa: 23/07/2025

Muhusika: Imaam Abu Bakr Ahmad bin Abiy ´Aaswim ash-Shaybaaniy (a.f.k. 287)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Kitaab-uz-Zuhd, uk. 66-68
Imechapishwa: 23/07/2025
https://firqatunnajia.com/68-kinga-dhidi-ya-mtihani-wa-dunia-na-adhabu-ya-ndani-ya-kaburi/