Wanazuoni wamesema kuwa inapendekezwa kuboresha sauti katika kusoma na kusoma kwa utaratibu na ipasavyo muda wa kuwa haitoki katika mipaka ya usomaji kwa kupitiliza kurefusha. Ikiwa atazidisha mpaka ambapo akaongeza herufi au akaificha, basi hilo ni haramu.
Ama kusoma kwa mizani ya nyimbo, ash-Shaafi´iy (Rahimahu Allaah) amesema katika sehemu moja ya kwamba anachukizwa na jambo hilo. Wakati mwingine amesema kuwa hachukizwi na jambo hilo. Maswahiba wetu wamesema kuwa hayo sio maoni mawili tofauti, bali ni jambo linahitaji ufafanuzi. Ikiwa atazidisha katika kurefusha mpaka akavuka mipaka, basi hilo ndilo lililochukiwa, na ikiwa hakuvuka mipaka, basi hilo ndilo lisilochukiwa. al-Mardaawiy amesema katika kitabu chake ”al-Haawiy”:
”Kusoma kwa melodi zilizotungwa, ikiwa kunabadilisha matamshi ya Qur-aan kwa kuingiza sauti za vokali ndani yake, kuondoa sauti za vokali, kufupisha yaliyorefushwa, kurefusha yaliyofupishwa, kurefusha kupita kiasi mpaka baadhi ya lafudhi zikafichika na maana kuchanganyika, basi hilo ni haramu. Msomaji anakuwa fasiki na msikilizaji anapata dhambi, kwa sababu ameiondoa katika njia yake iliyo sawa kwenda kwenye kupinda. Allaah (Ta´ala) amesema:
قُرْآنًا عَرَبِيًّا غَيْرَ ذِي عِوَجٍ
”… Qur-aan ya kiarabu isiyo na kombo.”[1]
[…] ikiwa melodi haiondoi lafudhi yake wala usomaji wake wa utaratibu ipasavyo, basi inajuzu, kwa sababu ameongeza uzuri katika sauti yake.”
Aina hii ya kwanza ya kusoma kwa melodi iliyo haramu ni msiba uliowapata baadhi ya wajinga wabaya ambao wanaosoma kwenye mazishi na baadhi ya mikusanyiko. Hii ni Bid´ah ya haramu iliyo wazi. Kama alivyosema al-Mardaawiy. Anapata dhambi kila anayesikiliza na anapata dhambi kila mwenye uwezo wa kuiondoa au kuikataza ikiwa hafanyi hivyo. Nimejitahidi kwa uwezo wangu katika hilo. Ninatarajia kwa fadhilah ya Allaah Mkarimu amuwezeshe kuiondoa yule anayestahiki na amfanye awe katika usalama.
Katika ”al-Mukhtaswar” ya al-Muzaniy imekuja ya kwamba ash-Shaafi´iy (Rahimahu Allaah) amesema:
”Aboreshe sauti yake kwa namna yoyote awezayo.”
Amesema kuwa anapenda zaidi kusoma kwa sauti ya haraka kiasi na ya huzuni. Wataalamu wa lugha wamesema kuwa kusoma kwa sauti ya haraka kunakusudiwa ikiwa umesoma kwa kuifuatiliza bila kuirefusha kupita kiasi. Kusoma kwa sauti ya huzuni kunamaanishwa ikiwa anailainisha sauti yake. Ibn Abiy Daawuud amepokea kwamba Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) alisoma “at-Takwiyr” katika hali ya huzuni kama mfano wa maombolezo. Abu Daawuud amepokea kwamba ´Ubaydullaah bin Abiy Yaziyd amesema:
”Nilimuuliza Ibn Abiy Mulaykah: ”Unaonaje ikiwa mtu hana sauti nzuri?” Akasema: ”Aiboreshe kadiri awezavyo.”[2]
[1] 39:28
[2] Abu Daawuud (1471). Nzuri na Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh Sunan Abiy Daawuud” (1471).
- Muhusika: Imaam Yahyaa bin Sharaf an-Nawawiy (afk. 677)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Tibyaan fiy Aadaabi Hamalat-il-Qur-aan, uk. 69-70
- Imechapishwa: 26/11/2026

Muhusika: Imaam Yahyaa bin Sharaf an-Nawawiy (afk. 677)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Tibyaan fiy Aadaabi Hamalat-il-Qur-aan, uk. 69-70
Imechapishwa: 26/11/2026
https://firqatunnajia.com/67-sharti-la-kuboresha-sauti-wakati-wa-kusoma-qur-aan/