Wanazuoni wameafikiana (Radhiya Allaahu ´anhum) miongoni mwa Salaf na waliokuja baada yao, kutoka kwa Maswahabah, wanafunzi wa Maswahabah na wanazuoni wa miji, maimamu wa waislamu, juu ya kupendekezwa kuboresha sauti kwa ajili ya Qur-aan. Maneno yao na matendo yao ni yenye kutambulika vyema kabisa, kwa ajili hiyo hatuhitaji kunukuu kila moja. Dalili ya hayo kutoka kwa Hadiyth za Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni nyingi kwa watu maalum na wa kawaida. Mfano wa Hadiyth inayosema:
“Pambeni Qur-aan kwa sauti zenu.”
“Hakika umepewa sauti nzuri miongoni mwa sauti nzuri za Daawuud.”
“Allaah hajasikiliza chochote kama vile anavyomsikiliza Nabii mwenye sauti nzuri akisoma Qur-aan kwa sauti.”
”Allaah humsikiliza kwa makini zaidi mtu mwenye sauti nzuri akisoma Qur-aan kwa sauti kuliko mmiliki mwanamke anayemsikiliza kijakazi wake.”
Yote haya yamekwishatangulia katika kipengele kilichotangulia. Pia imetangulia Hadiyth ya ´Abdullaah bin Mughaffal (Radhiya Allaahu ´anh) katika fadhilah za kusoma kwa utaratibu na ipasavyo, nayo ni:
”Nilimuona Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) siku ya kufunguliwa kwa mji wa Makkah akiwa juu ya ngamia wake akisoma Suurah al-Fath, akirudia kuipamba sauti yake katika usomaji wake.”
Vivyo hivyo Hadiyth ya Sa´d bin Abiy Waqqaas na Hadiyth ya Abu Lubaabah kuhusu kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Yule ambaye haimbi kwa Qur-aan si katika sisi.”[1]
Ameipokea Abu Daawuud kwa cheni mbili nzuri. Katika cheni ya wapokezi ya Hadiyth ya Sa´d kuna tofauti ambayo haidhuru. Wamesema wanazuoni wengi kwamba “Yule ambaye haimbi kwa Qur-aan si katika sisi” maana yake ni kwamba haipambi sauti yake wakati anaposoma.
Kadhalika al-Baraa´ (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:
”Nilimsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisoma katika ´Ishaa Suurah ”at-Tiyn”. Sikuwahi kusikia mtu mwenye sauti nzuri zaidi yake.”[2]
Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.
[1] Abu Daawuud (1471). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh Sunan Abiy Daawuud” (1471).
[2] al-Bukhaariy (769) na Muslim (464).
- Muhusika: Imaam Yahyaa bin Sharaf an-Nawawiy (afk. 677)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Tibyaan fiy Aadaabi Hamalat-il-Qur-aan, uk. 68-69
- Imechapishwa: 26/11/2026

Muhusika: Imaam Yahyaa bin Sharaf an-Nawawiy (afk. 677)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Tibyaan fiy Aadaabi Hamalat-il-Qur-aan, uk. 68-69
Imechapishwa: 26/11/2026
https://firqatunnajia.com/66-mapendezo-ya-kuboresha-sauti-wakati-wa-kusoma-qur-aan/