67. Safari katika njia ya Allaah ni bora kuliko ulimwengu na vyote vilivyomo ndani yake

237 – Ya´quub bin Humayd ametuhadithia: Marwaan bin Mu´aawiyah: Yahyaa bin Sa´iyd ametukhabarisha, kutoka kwa Abu Swaalih, kutoka kwa Abu Hurayrah, ambaye amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Safari ya jioni, au ya asubuhi, katika njia ya Allaah ni bora kuliko ulimwengu na vyote vilivyomo ndani yake.”[1]

238 – Abu Bakr ametukhabarisha: Abu Khaalid al-Ahmar ametukhabarisha, kutoka kwa Ibn ´Ajlaan, kutoka kwa Abu Haazim, kutoka kwa Abu Hurayrah, ambaye amesimulia kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Safari ya jioni, au ya asubuhi, katika njia ya Allaah ni bora kuliko ulimwengu na vyote vilivyomo ndani yake.”[2]

239 – Mpwa wa Juwayriyah ametukhabarisha: ´Abdullaah bin al-Mubaarak ametuhadithia, kutoka kwa adh-Dhwahhaak bin ´Uthmaan: al-Hakam bin Miynaa amenihadithia: Nimemsikia Abu Hurayrah, kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) mfano wa hayo.

240 – Abu Bakr ametukhabarisha: Wakiy´ ametukhabarisha: Sufyaan ametukhabarisha, kutoka kwa Abu Haazim, kutoka kwa Sahl bin Sa´d: Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema mfano wa hayo.

241 – Ibn Kaasib ametukhabarisha: Ibn Abiy Haazim ametukhabarisha, kutoka kwa baba, kutoka kwa Sahl, ambaye amesimulia kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Safari ya jioni, au ya asubuhi, ambayo mja anashika katika njia ya Allaah ni bora kuliko ulimwengu na vyote vilivyomo ndani yake.”

242 – Hudbah bin Khaalid ametukhabarisha: Hammaad bin Salamah ametukhabarisha, kutoka kwa Thaabit, kutoka kwa Anas, ambaye amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Safari ya jioni, au ya asubuhi, katika njia ya Allaah ni bora kuliko ulimwengu na vyote vilivyomo ndani yake.”

243 – Mpwa wa Juwayriyah: Ibn-ul-Mubaarak ametukhabarisha, kutoka kwa Muusa… (ح) ´Abdul-Wahhaab ametukhabarisha: ash-Shaafi´iy ametukhabarisha: al-Haarith bin ´Umayr ametukhabarisha … al-Maqdamiy ametukhabarisha pia: al-Mu´tamir bin Sulaymaan ametukhabarisha, kutoka kwa Humayd, kutoka kwa Anas, kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) mfano wa hayo.

244 – Abu Bakr na Abu Muusa wametukhabarisha: ´Abdullaah bin Yaziyd Abu ´Abdir-Rahmaan al-Muqri’ ametukhabarisha, kutoka kwa Sa´iyd bin Abiy Ayyuub: Shurahbiyl bin Shariyk al-Mu´aafariy ametukhabarisha, kutoka kwa Abu ´Abdir-Rahmaan al-Hubuliy: Nimemsikia Abu Ayyuub ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Safari ya jioni, au ya asubuhi, katika njia ya Allaah ni bora kuliko vyote vilivyochomozewa na jua.”[3]

245 – Abu Bakr bin Abiy Shaybah ametuhadithia: Abu Khaalid al-Ahmar ametukhabarisha, kutoka kwa al-Hajjaaj, kutoka kwa al-Hakam, kutoka kwa Muqsim, kutoka kwa Ibn ´Abbaas, kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), ambaye amesema:

“Safari ya jioni, au ya asubuhi, katika njia ya Allaah ni bora kuliko ulimwengu na vyote vilivyomo ndani yake.”

246 – Abu Muusa ametuhadithia: Wahb bin Jariyr ametukhabarisha: Baba yangu ametukhabarisha: Nimemsikia Yahyaa bin Ayyuub akisimulia kutoka kwa Yaziyd bin Abiy Habiyb, kutoka kwa Suwayd bin Qays, kutoka kwa Mu´aawiyah bin Hudayj, ambaye amesimulia kuwa amemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:

“Safari ya jioni, au ya asubuhi, katika njia ya Allaah ni bora kuliko ulimwengu wote.”[4]

247 – ´Uqbah bin Mukram ametukhabarisha: ´Abdul-Ghaffaar bin Daawuud ametuhadithia: Ibn Lahiy´ah ametukhabarisha, kutoka kwa Abul-Aswad, kutoka kwa ´Urwah bin az-Zubayr na Sulaymaan bin Yasaar, kutoka kwa Abu Hurayrah, ambaye amesimulia kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Safari ya jioni, au ya asubuhi, katika njia ya Allaah ni bora kuliko vyote vilivyochomozewa na kuzamiwa na jua.”

248 – ´Aliy bin Maymuun ametukhabarisha: ´Abdullaah bin Khaalid, ambaye ni ´Abduun al-Qarqasaaniy, ametukhabarisha, kutoka kwa ´Abdullaah bin Yaziyd bin Aadam, kutoka kwa Abud-Dardaa’, ambaye amesimulia kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Safari ya asubuhi, au ya jioni, katika njia ya Allaah ni bora kuliko vyote ambavyo jua na mwezi vimewahi kuchomoza juu yake pamoja na neema zake mpaka kitaposimama Qiyaamah.”

249 – Sa´iyd bin Yahyaa bin Sa´iyd al-Umawiy ametukhabarisha: Baba yangu ametukhabarisha: Muhammad bin ´Amr ametukhabarisha, kutoka kwa Abu Salamah, kutoka kwa Abu Hurayrah, ambaye ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakika mawalii katika nyinyi ni wale wanaomcha Allaah. Hebu msiache wakawepo watu wataokuja na matendo siku ya Qiyaamah, nanyi mnakuja na ulimwengu ambao mmeubeba juu ya shingo zenu na kusema: ”Ee Muhammad!” Kisha nitafanya hivi na hivi’ na akageuza uso wake upande.”[5]

[1] Muslim (1882).

[2] at-Tirmidhiy (1649). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh Sunan at-Tirmidhiy” (1649).

[3] al-Bukhariy (2793) na Muslim (1883).

[4] Ahmad (26711).

[5] Nzuri kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Dhwilaal-ul-Jannah” (213).

  • Muhusika: Imaam Abu Bakr Ahmad bin Abiy ´Aaswim ash-Shaybaaniy (a.f.k. 287)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-uz-Zuhd, uk. 64-66
  • Imechapishwa: 23/07/2025