Katika kio kuna taa. Nayo ni nuru iliyoko kwenye utambi. Nuru hiyo ina chanzo. Chanzo hicho ni mafuta yaliyochujwa kutoka kwenye mzeituni uliopo katika sehemu iliyo bora zaidi ambayo inapatwa na jua mwanzo na mwisho wa mchana. Mafuta yake ni safi zaidi na mbali zaidi na uchafu, kiasi kwamba karibu yang’ae yenyewe bila moto. Huu ndio asili ya nuru ya taa.
Vivyo hivyo chanzo cha nuru ya taa iliyo katika moyo wa muumini ni kutoka katika mti wa wahy ambao ndio kitu kilicho na baraka zaidi na kilicho mbali zaidi na upotofu. Bali ni kitu kilicho katikati ya mambo, kilicho sawa zaidi na bora zaidi. Haukupotoka kwa upotofu wa kikristo wala upotofu wa kiyahudi. Bali uko katikati ya pande mbili zilizosemwa vibaya katika kila jambo. Huu ndio msingi wa taa ya imani katika moyo wa muumini. Kwa kuwa yale mafuta yamekuwa safi sana kiasi kwamba karibu yang’ae yenyewe, kisha yakakutana na moto, basi mwangaza wake ukazidi kwa moto huo na nuru ya moto ikatiwa nguvu kwa mafuta hayo, basi matokeo yake ni nuru juu ya nuru.
Hivyo ndivyo ilivyo kwa moyo wa muumini unaoangaza. Anakaribia kuitambua haki kwa maumbile na akili yake. Lakini hana chanzo kutoka kwake mwenyewe. Ndipo kukaja chanzo cha wahy, kikachanganyika na moyo wake na kukutana na nuru yake. Matokeo yake nuru ikazidi kwa wahy juu ya nuru ya maumbile ambayo Allaah (Ta´ala) amemuumba kwayo. Hivyo ikakusanyika kwake nuru ya wahy na nuru ya maumbile – ikawa ni nuru juu ya nuru. Matokeo yake anakaribia atamke haki hata kama hajasikia masimulizi yoyote, halafu akasikia masimulizi kwa yale yanayoenda sambamba na maumbile yake, kwa hiyo inakuwa nuru juu nuru. Hivo ndivyo anakuwa muumini ambaye kwa jumla anaitambua haki kwa maumbile yake, kisha anasikia masimulizi juu yake kwa njia ya upambanuzi. Matokeo yake imani yake inakuwa kwa kushuhudia wahy na maumbile.
- Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 122-123
- Imechapishwa: 24/08/2025
Katika kio kuna taa. Nayo ni nuru iliyoko kwenye utambi. Nuru hiyo ina chanzo. Chanzo hicho ni mafuta yaliyochujwa kutoka kwenye mzeituni uliopo katika sehemu iliyo bora zaidi ambayo inapatwa na jua mwanzo na mwisho wa mchana. Mafuta yake ni safi zaidi na mbali zaidi na uchafu, kiasi kwamba karibu yang’ae yenyewe bila moto. Huu ndio asili ya nuru ya taa.
Vivyo hivyo chanzo cha nuru ya taa iliyo katika moyo wa muumini ni kutoka katika mti wa wahy ambao ndio kitu kilicho na baraka zaidi na kilicho mbali zaidi na upotofu. Bali ni kitu kilicho katikati ya mambo, kilicho sawa zaidi na bora zaidi. Haukupotoka kwa upotofu wa kikristo wala upotofu wa kiyahudi. Bali uko katikati ya pande mbili zilizosemwa vibaya katika kila jambo. Huu ndio msingi wa taa ya imani katika moyo wa muumini. Kwa kuwa yale mafuta yamekuwa safi sana kiasi kwamba karibu yang’ae yenyewe, kisha yakakutana na moto, basi mwangaza wake ukazidi kwa moto huo na nuru ya moto ikatiwa nguvu kwa mafuta hayo, basi matokeo yake ni nuru juu ya nuru.
Hivyo ndivyo ilivyo kwa moyo wa muumini unaoangaza. Anakaribia kuitambua haki kwa maumbile na akili yake. Lakini hana chanzo kutoka kwake mwenyewe. Ndipo kukaja chanzo cha wahy, kikachanganyika na moyo wake na kukutana na nuru yake. Matokeo yake nuru ikazidi kwa wahy juu ya nuru ya maumbile ambayo Allaah (Ta´ala) amemuumba kwayo. Hivyo ikakusanyika kwake nuru ya wahy na nuru ya maumbile – ikawa ni nuru juu ya nuru. Matokeo yake anakaribia atamke haki hata kama hajasikia masimulizi yoyote, halafu akasikia masimulizi kwa yale yanayoenda sambamba na maumbile yake, kwa hiyo inakuwa nuru juu nuru. Hivo ndivyo anakuwa muumini ambaye kwa jumla anaitambua haki kwa maumbile yake, kisha anasikia masimulizi juu yake kwa njia ya upambanuzi. Matokeo yake imani yake inakuwa kwa kushuhudia wahy na maumbile.
Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 122-123
Imechapishwa: 24/08/2025
https://firqatunnajia.com/67-nuru-juu-ya-nuru/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket