Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:
2 – Utashi wa Allaah (Ta´ala) unaotendeka na uwezo Wake wenye kuenea. Nako ni kule kuamini ya kwamba atakayo Allaah, huwa, na asiyotaka, hayawi. Hakuna mbinguni wala ardhini katika vinavyotikisika wala vilivyotulia isipokuwa vinakuwa kwa matakwa ya (Subhaanah). Hakukuwi katika ufalme Wake kile asichokitaka. Yeye (Subhaanah) ni Muweza wa kila jambo, ni mamoja yalioko na yasiokuwepo. Hakuna kimechoumbwa katika ardhi wala mbinguni isipokuwa Allaah (Subhaanah) ndiye kakiumba. Hakuna Muumbaji mwengine asiyekuwa Yeye na wala hakuna Mola asiyekuwa Yeye.
MAELEZO
Ngazi hii ina vipengele viwili pia: matakwa na uumbaji. Matakwa ya Allaah ni yenye kutekelezeka. Yale anayotaka Allaah, huwa, na yale asiyotaka hayawi. Yeye (Jalla wa ´Alaa) ndiye Muumbaji wa kila kitu. Amesema (Ta´ala):
وَمَا تَشَاءُونَ إِلَّا أَن يَشَاءَ اللَّـهُ رَبُّ الْعَالَمِينَ
“Na hamtotaka isipokuwa atake Allaah, Mola wa walimwengu.” (81:29)
اللَّـهُ خَالِقُ كُلِّ شَيْءٍ
“Allaah ndiye Muumbaji wa kila kitu.” (13:16)
Hakika Yeye (Subhaanah) aliyajua mambo, akayaandika na akayaumba. Yale anayotaka Allaah, huwa, na yale asiyotaka hayawi.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh al-´Aqiydah al-Waasitwiyyah, uk. 102-103
- Imechapishwa: 03/11/2024
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)