67. Du´aa wakati upepo unapovuma na kuwa mkali

155 – ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa), mkewe Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), amesimulia: “Alikuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) unapokuwa upepo mkali husema:

اللّهُـمَّ إِنَّـي أَسْـأَلُـكَ خَيْـرَها، وَخَيْـرَ ما فيهـا، وَخَيْـرَ ما اُرْسِلَـتْ بِه، وَأَعـوذُ بِكَ مِنْ شَـرِّها، وَشَـرِّ ما فيهـا، وَشَـرِّ ما اُرْسِلَـتْ بِه

”Ee Allaah! Nakuomba kheri yake, kheri ya kilichomo ndani yake na kheri ya iliyotumwa ndani yake. Na najilinda Kwako kutokamana na shari yake, shari ya kilichomo ndani yake na shari iliyotumwa nao.”[1]

Ameipokea Muslim.

MAELEZO

Katika Hadiyth hii kuna mapendezo ya kusoma du´aa hii wakati upepo unapovuma na kuwa mkali. Kumepokelewa makatazo ya kutukana upepo, kwani ni wenye kuamrishwa na kuendeshwa na Allaah (´Azza wa Jall).

[1] Muslim (899).

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 147
  • Imechapishwa: 16/11/2025