236 – Hishaam bin ´Amaarah ametuhadithia: Ismaa´iyl bin ´Ayyaash ametukhabarisha: ´Amaarah bin Ghaziyyah ametukhabarisha, kutoka kwa Rabiy´ah bin ´Abdir-Rahmaan, kutoka kwa ´Abdul-Malik bin Sa´iyd al-Answaariy, kutoka kwa Abu Usayd, ambaye amesimulia kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Fanyeni vizuri katika kuitafuta dunia. Kwani kila mmoja amewepesishiwa kwa kile alichoumbiwa kutokana nayo.” [1]

[1] Ibn Maajah (2142). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb” (1699).

  • Muhusika: Imaam Abu Bakr Ahmad bin Abiy ´Aaswim ash-Shaybaaniy (a.f.k. 287)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-uz-Zuhd, uk. 63
  • Imechapishwa: 22/07/2025