66. Elimu zinazohusiana na Qiyaamah zinatambulika kupitia wahy peke yake

Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:

Fafanuzi za hayo yote na hatua mbalimbali zilizokuja kuhusu Nyumba ya ´Aakhirah na mengine yote yanayohusiana na hesabu, malipo, adhabu, Pepo na Moto yametajwa ndani ya Vitabu vilivyoteremshwa kutoka mbinguni na elimu iliyopokelewa kutoka kwa Mitume. Na katika elimu iliyorithiwa kutoka kwa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuhusu hayo kuna yanayokinaisha na kutosheleza. Kwa yule mwenye kuyatafuta atayapata.

MAELEZO

Kuhusiana na fafanuzi za siku ya Qiyaamah, yanayohusiana na mizani, hali za mizani na uzito wake, namna ambavyo madaftari pia yatapimwa na mengineyo yote haya yametajwa ndani ya Qur-aan na ndani ya Hadiyth ambazo ni Swahiyh. Yule mwenye kuyataka kwa kina anaweza kuyapata.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-´Aqiydah al-Waasitwiyyah, uk. 98
  • Imechapishwa: 02/11/2024