66. Du´aa ya waliohai na swadaqah zao zinawanufaisha wafu

Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

107 – Du´aa ya waliohai na swadaqah zao zinawanufaisha wafu.

MAELEZO

Ibn Abiyl-´Izz (Rahimahu Allaah) amenakili maafikiano ya Ahl-us-Sunnah juu ya suala hilo na kisha akataja dalili ndani ya Qur-aan na Sunnah. Hata hivyo katika yanayohusiana na swadaqah hakutaja isipokuwa tu yale yanayofahamisha kuwa baba ndiye anayenufaika na swadaqah ya mtoto wake, jambo ambalo ni maalum zaidi kuliko madai yote. Nimebainisha suala hili na kulihoji juu ya makubaliano yaliyotajwa katika “Ahkaam-ul-Janaa’iz”[1].

[1] Tazama  “Ahkaam-ul-Janaa’iz”, uk. 173.

  • Muhusika: Sharh al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah – al-Albaaniy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah – Sharh wa Ta´liyq, uk. 99-100
  • Imechapishwa: 16/10/2024