145 – Sulaymaan bin Swurad (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia: “Waligombana watu wawili mbele ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambapo mmoja wao macho yake yakapiga wekundu na mishipa yake ya shingo ikasimama. Ndipo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Mimi najua neno ambalo akilisema basi ataondokewa na kile anachokihisi:
أَعُوذُ بِاللَّهِ مِنَ الشَّيْطَانِ الرَّجِيمِ
”Najilinda kwa Allaah kutokamana na shaytwaan aliyefukuzwa mbali na rehema za Allaah.”[1]
Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.
MAELEZO
Katika Hadiyth hii kuna uwekwaji Shari´ah wa kumwomba Allaah kinga dhidi ya shaytwaan aliyefukuzwa mbali wakati wa kuhisi hasira. Ayakariri pamoja na kuyafikiria na aidha kumdhania Allaah vyema, yakini na kurejea kwa Allaah. Ni jambo limewekwa katika Shari´ah akatawadha pia. Yote haya yamesuniwa kwa mtu wakati ameghadhabika. Vilevile kuketi chini ikiwa amesimama. Kutokana na uzoefu kutoka nje ya nyumba au yale maeneo alipo ni miongoni mwa mambo yanayoondoa ile hasira au kuepusha athari yake.
[1] al-Bukhaariy (6115) na Muslim (2610).
- Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 146
- Imechapishwa: 16/11/2025
145 – Sulaymaan bin Swurad (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia: “Waligombana watu wawili mbele ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambapo mmoja wao macho yake yakapiga wekundu na mishipa yake ya shingo ikasimama. Ndipo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Mimi najua neno ambalo akilisema basi ataondokewa na kile anachokihisi:
أَعُوذُ بِاللَّهِ مِنَ الشَّيْطَانِ الرَّجِيمِ
”Najilinda kwa Allaah kutokamana na shaytwaan aliyefukuzwa mbali na rehema za Allaah.”[1]
Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.
MAELEZO
Katika Hadiyth hii kuna uwekwaji Shari´ah wa kumwomba Allaah kinga dhidi ya shaytwaan aliyefukuzwa mbali wakati wa kuhisi hasira. Ayakariri pamoja na kuyafikiria na aidha kumdhania Allaah vyema, yakini na kurejea kwa Allaah. Ni jambo limewekwa katika Shari´ah akatawadha pia. Yote haya yamesuniwa kwa mtu wakati ameghadhabika. Vilevile kuketi chini ikiwa amesimama. Kutokana na uzoefu kutoka nje ya nyumba au yale maeneo alipo ni miongoni mwa mambo yanayoondoa ile hasira au kuepusha athari yake.
[1] al-Bukhaariy (6115) na Muslim (2610).
Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 146
Imechapishwa: 16/11/2025
https://firqatunnajia.com/66-duaa-wakati-wa-hasira/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket