Hakuna yeyote ambaye alikuwa anamuabudu Allaah peke yake ambaye atabaki Motoni. Wataobaki tu ni makafiri ambao Allaah amewafaradhishia kudumu humo milele. Amesema (Ta´ala):

كَذَٰلِكَ يُرِيهِمُ اللَّـهُ أَعْمَالَهُمْ حَسَرَاتٍ عَلَيْهِمْ ۖ وَمَا هُم بِخَارِجِينَ مِنَ النَّارِ

“Hivyo ndivyo Allaah atakavyowaonyesha matendo yao kuwa ni majuto juu yao. Na wala hawatokuwa wenye kutoka Motoni.” (02:167)

مَّأْوَاهُمْ جَهَنَّمُ كُلَّمَا خَبَتْ زِدْنَاهُمْ سَعِيرًا

“Makazi yao ni [moto wa] Jahannam, kila ukififia Tutawazidishia Moto uliowashwa vikali kwa ukali.” (17:97)

فَذُوقُوا فَلَن نَّزِيدَكُمْ إِلَّا عَذَابًا

“Basi onjeni – kwani Hatutokuzidishieni chochote isipokuwa adhabu!” (78:30)

يُرِيدُونَ أَن يَخْرُجُوا مِنَ النَّارِ وَمَا هُم بِخَارِجِينَ مِنْهَا ۖ وَلَهُمْ عَذَابٌ مُّقِيمٌ

“Watataka kutoka katika Moto lakini wao si wenye kutoka kamwe humo; na watapata adhabu ya kudumu.” (05:37)

وَهُمْ يَصْطَرِخُونَ فِيهَا رَبَّنَا أَخْرِجْنَا نَعْمَلْ صَالِحًا غَيْرَ الَّذِي كُنَّا نَعْمَلُ أَوَلَمْ نُعَمِّرْكُم مَّا يَتَذَكَّرُ فِيهِ مَن تَذَكَّرَ وَجَاءكُمُ النَّذِيرُ فَذُوقُوا فَمَا لِلظَّالِمِينَ مِن نَّصِيرٍ

“Nao watapiga mayowe humo: “Mola wetu, tutoe tutende mema mbali na ya yale tulIokuwa tukitenda!” [Ndipo Aseme:] “Je, kwani hatukukupeni umri wa kukumbuka mwenye kukumbuka humo? Na alikujieni mwonyaji! Basi onjeni [adhabu]! Kwani madhalimu hawana yeyote yule wa kuwanusuru!” (35:37)

Hii ndio itakuwa hali yao na mwisho wao. Ni adhabu ya milele na isiyokatika. Wataadhibiwa milele kwenye Moto usiokatika na hawatotolewa humo na ni Moto ambao hautozima.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-´Aqiydah al-Waasitwiyyah, uk. 97-98
  • Imechapishwa: 02/11/2024