Allaah amepiga mfano wa nuru ndani ya moyo wa mja Wake mfano ambao hawaufahamu isipokuwa tu watambuzi. Amesema (Subhaanahu wa Ta´ala):
اللَّـهُ نُورُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۚ مَثَلُ نُورِهِ كَمِشْكَاةٍ فِيهَا مِصْبَاحٌ ۖ الْمِصْبَاحُ فِي زُجَاجَةٍ ۖ الزُّجَاجَةُ كَأَنَّهَا كَوْكَبٌ دُرِّيٌّ يُوقَدُ مِن شَجَرَةٍ مُّبَارَكَةٍ زَيْتُونَةٍ لَّا شَرْقِيَّةٍ وَلَا غَرْبِيَّةٍ يَكَادُ زَيْتُهَا يُضِيءُ وَلَوْ لَمْ تَمْسَسْهُ نَارٌ ۚ نُّورٌ عَلَىٰ نُورٍ ۗ يَهْدِي اللَّـهُ لِنُورِهِ مَن يَشَاءُ ۚ وَيَضْرِبُ اللَّـهُ الْأَمْثَالَ لِلنَّاسِ ۗ وَاللَّـهُ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ
”Allaah ni Nuru ya mbingu na ardhi. Mfano wa Nuru Yake ni kama shubaka lenye kuwekwa ndani yake taa. Taa hiyo iko ndani ya gilasi. Gilasi hiyo ni kama nyota inayomeremeta, inayowashwa kutokana na mti wa baraka wa zaituni, si wa mashariki wala wa magharibi. Yanakaribia mafuta yake kung’aa ingawa moto haujayagusa. Nuru juu ya Nuru! Allaah anamuhidi kwa Nuru Yake amtakaye na Allaah anapiga mifano kwa watu. Allaah kwa kila jambo ni Mjuzi.”[1]
Ubay bin Ka´b amesema:
”Huu ndio mfano wa nuru Yake ndani ya moyo wa muislamu.”
Hii ndio nuru Aliyoitia ndani ya moyo wake katika kumtambua, kumpenda, kumwamini na kumtaja Kwake. Hiyo ndiyo nuru Yake Aliyoiteremsha kwao ambapo akawahuisha kwayo na kuwafanya kutembea nayo miongoni mwa watu. Asili yake ipo ndani ya mioyo yao kisha nguvu yake huongezeka hadi huonekana usoni mwao, viungo mwao, miilini mwao hadi kwenye mavazi na nyumba zao. Huyatambua haya mwenye kuwa wa aina yao. Viumbe wengine si wenye kuyatambua.
Siku ya Qiyaamah nuru hii itadhihiri waziwazi ikawa inaangaza mbele yao katika giza la Daraja mpaka wavuke. Nuru hiyo itaangaza kwa mujibu wa nguvu au udhaifu wa nuru hiyo katika mioyo yao walipokuwa ulimwenguni. Miongoni mwao ni mwenye nuru kama jua, wengine kama mwezi, wengine kama nyota, wengine kama taa. Wengine wanapewa nuru juu ya vidole vya miguu yao; mara huangaza na mara nyingine inazimika. Ikiwa hiyo ndio ilikuwa hali ya nuru yake ulimwenguni, basi hupata juu ya Daraja kwa kiasi hicho. Bali ni nuru ileile aliyokuwa akionekana kwayo kwa macho yake mwenyewe. Wakati mnafiki hakuwa na nuru thabiti ulimwenguni – bali nuru yake ilikuwa ya juujuu na si ya ndani – ndipo atapewa nuru ya juujuu tu ambayo mwisho wake ni giza na adhabu.
[1] 24:35
- Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 119-120
- Imechapishwa: 24/08/2025

Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 119-120
Imechapishwa: 24/08/2025
https://firqatunnajia.com/65-nuru-yako-duniani-ndio-inayokuamulia-nuru-yako-aakhirah/