65. Mtu wa kwanza atakayefufuka siku ya Qiyaamah

62 – Abu Sa´iyd ameeleza:

”Myahudi mmoja alimtaja Muusa kwa namna ya kwamba ni kana kwamba alimfadhilisha mbele ya Mtume wetu (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), ambapo yule Mnusuraji akampiga kofi. Myahudi yule akaja kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kumshtaki bwana yule, ambapo akasema: ”Msinifadhilishe mbele ya Mitume wengine. Mimi ndiye wa kwanza ambaye ardhi itamfufua. Tahamaki itakuwa ni Muusa ambaye ameishika moja ya nguzo za ´Arshi. Sijui kama yeye ndiye aliyefufuliwa wakati wa kuzimia mara ya kwanza au ni baada yangu.”

Muslim ameipokea kutoka kwake:

”Msifadhilishe kati ya Mitume.”[1]

[1] Uhakika wa mambo ni kwamba Muslim amepokea mfano wake kwa ukamilifu, lakini katika tamko lake amerejesha vilevile katika Hadiyth ya Abu Hurayrah iliotangulia. al-Bukhaariy pia ameipokea kwa ukamilifu wake katika maeneo mawili. Vivyo hivyo ndivo alivofanya Ahmad Ahmad (3/33) na Abu Daawuud (468) kwa ufupisho, na ipo vilevile kwa Ahmad (3/31).

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Mukhtasar-ul-´Uluww, uk. 108
  • Imechapishwa: 26/06/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy