234 – Abu Bakr ametukhabarisha: ´Affaan ametukhabarisha: Salaam Abul-Mundhir ametuhadithia, kutoka kwa Thaabit, kutoka kwa Anas, ambaye amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Nimependezewa mimi katika dunia wanawake na manukato na kitulizo cha jicho langu kimefanywa ni ndani ya swalah.”[1]

235 – Abu Kaamil ametuhadithia: Salaam bin Abiys-Swahbaa’ ametuhadithia, kutoka kwa Thaabit, kutoka kwa Anas, ambaye amesimulia kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Nimependezewa mimi katika dunia manukato na wanawake.”

[1] Ahmad, an-Nasaa’iy katika ”´Ishrat-un-Nisaa” (3939-3940), al-Haakim na al-Bayhaqiy. Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh-ul-Jaamiy´” (3124).

  • Muhusika: Imaam Abu Bakr Ahmad bin Abiy ´Aaswim ash-Shaybaaniy (a.f.k. 287)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-uz-Zuhd, uk. 63
  • Imechapishwa: 22/07/2025