Kwa sababu ya kumuiga Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) inapendekezwa kuingia Makkah kutoka upande wake wa juu na kuingia msikitini kupitia mlango wa Banuu Shaybah.
Anapouona msikiti wa Ka´bah huinua mikono yake na kusema:
الله أكبر
”Allaah ni mkubwa.”
na:
والحمد لله
”Himdi zote njema anastahiki Allaah.”
na humsifu na kumuomba.
Ikiwa mtu ni mwenye kufanya ´Umrah, basi huanza kufanya Twawaaf ya ´Umrah. Ikiwa mtu ni mwenye kufanya Hajj ya Ifraad au Hajj ya Qiraan, basi huanza na Twawaaf ya kuwasili (طواف القدوم).
Kisha huvaa shuka yake ya juu yake kwa namna ya kuweka sehemu yake ya katikati chini ya kwapa lake la kulia na ncha zake mbili juu ya bega lake la kushoto.
Kisha huanza kwenye Jiwe Jeusi, huligusa na kulibusu na husema:
بسم الله والله أكبر، اللهم إيمانًا بك، وتصديقًا بكتابك، ووفاءً بعهدك، واتباعًا لسنة نبيك محمد
“Kwa jina la Allaah, Allaah ni mkubwa. Ee Allaah! Kwa kukuamini Wewe, kuithibitisha Kitabu Chako, kutimiza ahadi Yako na kufuata Sunnah za Mtume Wako Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).”
Kisha huzunguka Ka´bah upande wake wa kulia na huifanya Ka´bah iwe upande wake wa kushoto. Hufanya Twawaaf mara saba, akienda kwa mwendo wa haraka katika mara tatu za mwanzo kutoka kwenye Jiwe Jeusi mpaka kwenye Jiwe Jeusi na akitembea katika mara nne zilizobaki.
Kila anapolingana na kona ya kiyemeni na Jiwe Jeusi, basi huvigusa na kusema:
الله أكبر
”Allaah ni mkubwa.”
na:
لا إله إلا الله
”Hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah.”
na husema baina ya kona ya kiyemeni na Jiwe Jeusi:
ربنا آتنا في الدنيا حسنة وفي الآخرة حسنة وقنا عذاب النار
“Ee Mola wetu! Tupe duniani wema na Tupe Aakhirah wema na tukinge na adhabu ya Moto!”[1]
Huomba katika sehemu nyingine za Twawaaf kwa chochote anachokipenda.
Kisha huswali Rak´ah mbili nyuma ya Mahali pa kusimama na kuomba du´aa.
Kisha hurudi kwenye kona na kuigusa.
Halafu hutoka kwenda Swafaa kupitia mlango wake, hupanda juu yake, husema sentesi kama:

na kumuomba.
Kisha hushuka na kutembea mpaka kwenye alama, kisha hukimbia mpaka kwenye alama nyingine, kisha hutembea mpaka anapofika Marwah. Hufanya hapo kama alivyofanya juu ya Swafaa. Kisha hushuka na kutembea katika sehemu ya kutembea na hukimbia katika sehemu ya kukimbia, mpaka anakamilisha mizunguko saba. Huhesabu kwenda kuwa ni Sa´y moja, na kurudi kuwa ni Sa´y nyingine. Huanzia kwa Swafaa na humalizia kwa Marwah.
Kisha ikiwa ni mwenye kufanya ´Umrah, basi hupunguza nywele zake na huwa ametoka katika Ihraam. Isipokuwa mwenye kufanya Hajj ya Tamattu´ ikiwa ana mnyama wa Hadiy, mwenye kufanya Hajj ya Qiraan na Hajj ya Ifraad. Hawa hawatoki katika Ihraam.
Mwanamke ni kama mwanaume, isipokuwa yeye hakimbii kwa mwendo wa haraka katika Twawaaf wala katika Sa´y.
[1] 02:201
- Muhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy (afk. 620)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: ´Umdat-ul-Fiqh, uk. 46-47
- Imechapishwa: 09/11/2026

Muhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy (afk. 620)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: ´Umdat-ul-Fiqh, uk. 46-47
Imechapishwa: 09/11/2026
https://firqatunnajia.com/65-kuingia-makkah/