Swali: Baada ya kukojoa, kwa maana nyingine baada ya mkojo kutoka, hubaki matone ya mkojo kwenye uume. Mimi hukaa karibu robo saa bafuni ili nijisafishe vizuri kutokana na mkojo. Bila shaka jambo hili hunichosha na kuniletea usumbufu. Baada ya hapo hutawadha kwa ajili ya swalah. Nimekwenda kwa madaktari kadhaa, ambapo nikafanyiwa vipimo na kutumia aina mbalimbali za dawa kwa ajili ya kuondokana na hali hii, lakini bila kufua dafu. Baada ya kujisafisha vizuri kutokana na matone ya mkojo yaliyobaki, hutawadha na kwenda kuswali. Wakati wa swalah nahisi kana kwamba bado kuna matone ya mkojo kwenye uume yanayotaka kutoka. Bila shaka jambo hili huniletea matatizo na kunitia uzito, khaswa ninaposwali kwa mkusanyiko. Baada ya swalah hugundua kwamba kuna matone ya mkojo yaliyobaki ambayo huenda yasitoke haraka ninapokuwa nimekaa bafuni na hivyo hulazimika kurudia swalah au huwa na shaka kwamba swalah yangu si sahihi.
Jibu: Ikiwa umetawadha, basi msingi ni kwamba una twahara. Kwa hivyo usizingatie shaka na wasiwasi unaokujia. Hayo yanatokana na shaytwaan. Ni kweli kwamba ikiwa utakuwa na yakini kwamba kitu kimetoka kwako baada ya wudhuu´, basi wudhuu´ wako unabatilika na ni wajibu kwako kutawadha tena. Vivyo hivyo kuhusu unachohisi wakati wa swalah kwamba kuna mabaki ya mkojo kwenye uume, unatakiwa kujishughulisha na jambo jingine na kujenga juu ya msingi wa kuwa una twahara. Huhitaji kujichunguza baada ya hapo, kwa sababu kufanya hivyo kunasababisha wasiwasi huo kuendelea. Allaah akuponye na hilo.
- Muhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (5/227-228)
- Imechapishwa: 09/11/2026

Muhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (5/227-228)
Imechapishwa: 09/11/2026
https://firqatunnajia.com/anabaki-chooni-mwa-muda-mrefu-kwa-kuhisi-mkojo-hujatoka-vizuri/