103 – Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ameeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema: “Ikiwa mmoja wenu atamwingilia mke wake atasema:

اللَّهُمَّ جَنِّبْنَا الشَّيْطَانَ وَجَنْبِ الشَّيْطَانَ مَا رَزَقْتَنَا

“Ee Allaah! Tulinde na shaytwaan na Kilinde na shaytwaan kile utachoturuzuku.”

kisha wakahukumiwa kupata mtoto, basi hatomdhuru.”[1]

Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.

MAELEZO

Katika Hadiyth hii kuna dalili ya uwekwaji Shari´ah kwa mwanaume kutaja jina la Allaah kabla ya kumjamii mke wake.

Jengine ni kwamba ndani ya jina la Allaah kuna faida kuu. Nayo ni Allaah kuwaepusha na shaytwaan na kwamba Allaah akiwakadiria kupata mtoto basi anakuwa ni mwenye kuhifadhiwa kutokana na shaytwaan na hivyo hamdhuru. Muislamu ayafanye haya kwa kufuata Sunnah na amjengee dhana nzuri Allaah (´Azza wa Jall).

[1] al-Bukhaariy (141) na Muslim (1434).

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 145
  • Imechapishwa: 16/11/2025