61 – Abu Hurayrah ameeleza:

”Aligombana bwana mmoja katika waislamu na bwana mmoja katika mayahudi, ambapo muislamu yule akasema: ”Naapa kwa Yule ambaye amemchagua Muhammad juu ya walimwengu wote!” Myahudi yule akasema: ”Naapa kwa Yule ambaye amemchagua Muusa juu ya walimwengu wote!” Muislamu yule akampa kofi yule myahudi ambapo myahudi yule akaenda kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kumweleza. Ndipo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: ”Msinifadhilishe juu ya Muusa! Wakati watu watapozimia mimi ndiye wa kwanza nitayepata fahamu, tahamaki nimuone Muusa ameshasimama na ameshika ubavu wa ´Ashi. Sijui kama alikuwa miongoni mwa waliozimia na akapata fahamu kabla yangu au ni miongoni mwa wale ambao wamebaguliwa na Allaah (´Azza wa Jall).”

Imekuja katika upokezi mwingine kutoka kwake (Radhiya Allaahu ´anh):

”Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akaghadhibika na kusema: ”Msinifadhilishe mbele ya Mitume wa Allaah… Tahamaki Muusa ameishika ´Arshi. Sijui kama alipatwa na kuzirai siku ya Twuur au alifufuliwa kabla yangu.”

Imekuja katika tamko jengine:

”Kutapulizwa Baragumu ambapo wazirai wote waliyoko mbinguni na ardhini – isipokuwa wale awatakao Allaah. Kisha kupulizwe mara nyingine, ambapo tahamaki wasimame wakitazama. Mimi ndiye nitakuwa wa kwanza nitayefufuliwa – au miongoni mwa wale wa mwanzo watakaofufuliwa. Tahamaki Muusa ameishika ´Arshi. Sijui kama tayari ameshafanyiwa hesabu.”

Kuna maafikiano juu ya kuthibiti kwake.

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Mukhtasar-ul-´Uluww, uk. 107-108
  • Imechapishwa: 26/06/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy