232 – Hudbah bin Khaalid ametukhabarisha: Hammaad bin Salamah ametukhabarisha, kutoka kwa Sa´iyd al-Jariyriy, kutoka kwa Abu Nadhwrah, kutoka kwa ´Abdullaah bin Mawlah, kutoka kwa Buraydah, ambaye amesimulia kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Kinamtosha mmoja wenu katika ulimwengu mtumishi na nyumba.”[1]

233 – Abu Bakr ametuhadithia: Khalaf bin Khaliyfah ametukhabarisha, kutoka kwa Humayd bin ´Atwaa’, kutoka kwa ´Abdullaah bin al-Haarith, kutoka kwa ´Abdullaah bin Mas´uud, ambaye amesimulia kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Inashangaza jinsi mtu anaweza kuwa menye kughafilika lakini si mwenye kughafilishwa. Inashangaza jinsi mtu anavyoitafuta dunia ilihali kifo kinamtafuta. Inashangaza jinsi mtu anavyocheka kinywa chote bila ya yeye kujua kama Allaah amemridhia au amemkasirikia.”[2]

[1] Ahmad (22534). Nzuri kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh-ul-Jaamiy´” (5464).

[2] Dhaifu kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Dhwa´iyf-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb” (3680).

  • Muhusika: Imaam Abu Bakr Ahmad bin Abiy ´Aaswim ash-Shaybaaniy (a.f.k. 287)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-uz-Zuhd, uk. 62
  • Imechapishwa: 22/07/2025