152 – Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Anapochemua mmoja wenu, basi aseme:

الْحَمْـدُ للهِ

“Himdi zote ni stahiki ya Allaah.”

Ndugu au rafiki yake amwambie:

يَرْحَمُـكَ الله

“Allaah akurehemu.”

Atakapoambiwa hivo basi aseme tena:

يَهْـديكُـمُ اللهُ وَيُصْـلِحُ بالَـكُم

“Allaah awaongoze na ayatengeneze mambo yenu.”[1]

Ameipokea al-Bukhaariy.

MAELEZO

Katika Hadiyth kuna faida zifuatazo:

1 – Uwekwaji Shari´ah wa kumhimidi Allaah baada ya kuchemua kwa yeye kusema:

الحمد لله رب العالمين

“Himdi zote njema anastahiki Allaah, Mola wa walimwengu.”

au:

الحمد لله

“Himdi zote njema anastahiki Allaah.”

2 – Uwekwaji Shari´ah wa kumtakia rehema mchemuaji akimuhimidi Allaah kwa njia ya kwamba msemaji amwambie:

يَرْحَمُـكَ الله

“Allaah akurehemu.”

Asipomshukuru Allaah basi hatotakiwa rehema. Imepokelewa katika Hadiyth ya kwamba kuna watu wawili waliochemua mbele ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambapo akamtakia rehema yule mmoja na hakumtakia rehema yule mwingine. Akasema yule bwana ambaye hakumtakia rehema: “Amechemua fulani ukamtakia rehema na mimi nimechemua hukunitakia rehema. Ndipo akasema:

“Huyu amemuhimidi Allaah na wewe hukumuhimidi Allaah.”[2]

[1] al-Bukhaariy (6224).

[2] Muslim (2991).

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 144
  • Imechapishwa: 16/11/2025