231 – Hishaam bin ´Ammaar ametukhabarisha: al-Hakam bin Hishaam ametukhabarisha: Yahyaa bin Sa´iyd bin Abaan al-Qurashiy ametukhabarisha, kutoka kwa Abu Farwah, kutoka kwa Abu Khallaad, ambaye alikuwa Swahabah, ambaye amesimulia kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mkimuona muumini ambaye amepewa kuipa nyongo dunia na uchache wa kuzungumza, basi msogeleeni – kwani hakika amepewa hekima.”[1]

[1] Dhaifu kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Dhwa´iyf-ul-Jaamiy´” (4101).

  • Muhusika: Imaam Abu Bakr Ahmad bin Abiy ´Aaswim ash-Shaybaaniy (a.f.k. 287)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-uz-Zuhd, uk. 62
  • Imechapishwa: 21/07/2025