150 – ´Abdullaah bin ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesimulia kwamba alikuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anapopanda juu ya ngamia kwa ajili ya kusafiri husema:
الله أكبر ، الله أكبر ، الله أكبر سبحان الذي سخر لنا هذا وما كنا له مقرنين ، وإنا إلى ربنا لمنقلبون ، اللهم إنا نسألك في سفرنا هذا البر والتقوى ومن العمل ما ترضى ، اللهم هون علينا سفرنا هذا ، واطو عنا بعده ، اللهم أنت الصاحب في السفر ، والخليفة في الأهل ، اللهم إني أعوذ بك من وعثاء السفر ، وكآبة المنظر ، وسوء المنقلب ، في المال والأهل
”Allaah ni mkubwa. Allaah ni mkubwa. Allaah ni mkubwa. Ametakasika kutokamana na mapungufu ambaye ametuwepesishia haya na tusingeliweza wenyewe kuyadhibiti na hakika kwa Mola wetu tutarejea. Ee Allaah! Hakika sisi tunakuomba katika safari yetu hii wema na kukucha na katika matendo unayoyaridhia. Ee Allaah! Ifanye nyepesi safari yetu hii na fupisha umbali wake. Ee Allaah! Hakika Wewe ndiye unayesuhubiana nami katika safari na mchungaji wa familia yangu. Ee Allaah! Hakika mimi najilinda Kwako kutokamana na ugumu wa safari, ubaya wa mtizamo na mgeuko mbaya katika mali na familia.”
Anaporejea huyasema maneno hayo na akazidisha juu yake:
آيِبُـونَ تائِبُـونَ عابِـُدونَ لِرَبِّنا حـامِـدُونَ
”Tunarudi hali ya kuwa tunatubia na tunaabudu na hali ya kuwa ni wenye kumsifu Mola wetu.”[1]
Ameipokea Muslim.
151 – ´Abdullaah bin Sarjisa (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia:
“Alikuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisafiri basi anaomba kinga kutokamana na misukosuko ya safari, mgeuko mbaya, kurejea kutoka katika utiifu kwenda katika maasi, du´aa ya mwenye kudhulumiwa na mtizamo mbaya katika familia na mali.”[2]
Ameipokea Muslim.
MAELEZO
Katika Hadiyth hizi mbili kuna uwekwaji Shari´ah wa kuomba du´aa hii mtu anapokuwa safarimi.
Maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“… tusingeliweza wenyewe kuyadhibiti.”
Bi maana tusingeweza misukosuko yake kama si Allaah kutufanyia wepesi.

”Ee Allaah! Hakika sisi tunakuomba katika safari yetu hii wema… ”
Wema umefasiriwa kuwa ni kufanya yale maamrisho na ´uchaji` ni kuyaacha yale makatazo. Kukitajwa kimoja kwa kuachia basi kunaingia dini yote. Katika hayo ni maneno Yake (Ta´ala):
وَتَعَاوَنُوا عَلَى الْبِرِّ وَالتَّقْوَىٰ
“Saidianeni katika wema na uchaji Allaah.”[3]
Bi maana saidianeni katika kutekeleza maamrisho na kujiepusha na makatazo.

”Ee Allaah! Hakika mimi najilinda Kwako kutokamana na ugumu wa safari… ”
Ugumu ni ile misukosuko na tabu. Mgeuko ni ule huzuni unaopatikana kwa sababu ya kubadilika kwa muonekano huo.

“… mgeuko mbaya.”
Bi maana kurejea.

“…. kurejea kutoka katika utiifu kwenda katika maasi.”
Na kutoka katika imani kwenda katika ukafiri.
[1] Muslim (1342).
[2] Muslim (1343).
[3] 05:02
- Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 142-143
- Imechapishwa: 16/11/2025

Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 142-143
Imechapishwa: 16/11/2025
https://firqatunnajia.com/63-duaa-ya-safari-na-kutoka-safarini-2/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket