Wakati mwingine alikuwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anaweza kuketi mtindo wa al-Iq´aa’ ambapo anakalia visigino vyake na vidole vyake[1].
[1] Muslim, Abu ´Awaanah, Abuush-Shaykh katika ”Maa rawaahu Abuuz-Zubayr ´an Jaabir” (104-106) na al-Bayhaqiy. Ibn-ul-Qayyim (Rahimahu Allaah) amesahau pindi alipotaja kikao cha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) baina ya Sujuud mbili:
“Haikupokelewa ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliikaa kikao hichi kwa mtindo mwingine isipokuwa hichi tu.”
Ni vipi itakuwa sahihi ilihali al-Iq´aa’ imepokelewa kupitia Hadiyth ya Ibn ´Abbaas katika al-Bukhaariy, Abu Daawuud na at-Tirmidhiy aliyeisahihisha? Tazama “as-Swahiyhah” (383). Kadhalika Hadiyth hiyo imepokelewa na al-Bayhaqiy kwa mlolongo wa wapokezi mzuri kupitia kwa Ibn ´Umar ambayo imesahihishwa na Ibn Hajar. Abu Ishaaq al-Harbiy ameipokea katika “Ghariyb-ul-Hadiyth” (01/12/05) kutoka kwa Twaawuus ambaye anaonelea kuwa Ibn ´Umar na Ibn ´Abbaas walikaa mtindo wa al-Iq´aa’. Mlolongo wa wapokezi ni Swahiyh. Allaah amrehemu Imaam Maalik aliyesema: “Hakuna yeyote katika sisi isipokuwa maneno yake yanakubaliwa na kurudishwa isipokuwa huyu aliyemo ndani ya kaburi hili” na akaashiria kaburi la Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Sunnah hii ilitendewa kazi na Maswahabah wengi, Taabi´uun na wengineo. Hata hivyo al-Iq´aa’ hii sio ile iliyokatazwa, kama itavyokuja huko katika Tashahhud.
- Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Swifatu Swalaat-in-Nabiy, uk. 132
- Imechapishwa: 07/08/2017
Wakati mwingine alikuwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anaweza kuketi mtindo wa al-Iq´aa’ ambapo anakalia visigino vyake na vidole vyake[1].
[1] Muslim, Abu ´Awaanah, Abuush-Shaykh katika ”Maa rawaahu Abuuz-Zubayr ´an Jaabir” (104-106) na al-Bayhaqiy. Ibn-ul-Qayyim (Rahimahu Allaah) amesahau pindi alipotaja kikao cha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) baina ya Sujuud mbili:
“Haikupokelewa ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliikaa kikao hichi kwa mtindo mwingine isipokuwa hichi tu.”
Ni vipi itakuwa sahihi ilihali al-Iq´aa’ imepokelewa kupitia Hadiyth ya Ibn ´Abbaas katika al-Bukhaariy, Abu Daawuud na at-Tirmidhiy aliyeisahihisha? Tazama “as-Swahiyhah” (383). Kadhalika Hadiyth hiyo imepokelewa na al-Bayhaqiy kwa mlolongo wa wapokezi mzuri kupitia kwa Ibn ´Umar ambayo imesahihishwa na Ibn Hajar. Abu Ishaaq al-Harbiy ameipokea katika “Ghariyb-ul-Hadiyth” (01/12/05) kutoka kwa Twaawuus ambaye anaonelea kuwa Ibn ´Umar na Ibn ´Abbaas walikaa mtindo wa al-Iq´aa’. Mlolongo wa wapokezi ni Swahiyh. Allaah amrehemu Imaam Maalik aliyesema: “Hakuna yeyote katika sisi isipokuwa maneno yake yanakubaliwa na kurudishwa isipokuwa huyu aliyemo ndani ya kaburi hili” na akaashiria kaburi la Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Sunnah hii ilitendewa kazi na Maswahabah wengi, Taabi´uun na wengineo. Hata hivyo al-Iq´aa’ hii sio ile iliyokatazwa, kama itavyokuja huko katika Tashahhud.
Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Swifatu Swalaat-in-Nabiy, uk. 132
Imechapishwa: 07/08/2017
https://firqatunnajia.com/63-al-iqaa-kati-ya-sujuud-mbili/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)