Swali 62: Salafiyyah ni nini? Je, ni wajibu kufuata na kushikamana na mfumo wake?

Jibu: Salafiyyah ni kupita juu ya mfumo wa Salaf. Salaf walikuwa Maswahabah na wanafunzi wa Maswahabah na vile vizazi bora. Ni lazima kwa muislamu kuwafuata inapokuja katika ´Aqiydah, ufahamu na tabia[1]. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَالسَّابِقُونَ الْأَوَّلُونَ مِنَ الْمُهَاجِرِينَ وَالْأَنصَارِ وَالَّذِينَ اتَّبَعُوهُم بِإِحْسَانٍ رَّضِيَ اللَّـهُ عَنْهُمْ وَرَضُوا عَنْهُ وَأَعَدَّ لَهُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي تَحْتَهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًا ۚ ذَٰلِكَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ

“Wale waliotangulia mwanzoni ambao ni Muhaajiruun na Answaar na wale waliowafuata kwa wema, Allaah ameridhika nao nao wameridhika Naye na amewaandalia mabustani yapitayo chini yake mito – ni wenye kudumu humo milele. Huko ndiko kufuzu kukubwa.”[2]

وَالَّذِينَ جَاءُوا مِن بَعْدِهِمْ يَقُولُونَ رَبَّنَا اغْفِرْ لَنَا وَلِإِخْوَانِنَا الَّذِينَ سَبَقُونَا بِالْإِيمَانِ وَلَا تَجْعَلْ فِي قُلُوبِنَا غِلًّا لِّلَّذِينَ آمَنُوا رَبَّنَا إِنَّكَ رَءُوفٌ رَّحِيمٌ

”Na wale waliokuja baada yao wanasema: ”Ee Mola wetu! Tusamehe na ndugu zetu ambao wametutangulia kwa imani na wala Usijaalie katika nyoyo zetu mafundo ya chuki kwa wale walioamini; Mola wetu! Hakika Wewe ni Mwenye huruma mno, Mwenye kurehemu!”[3]

Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

”Lazimianeni na Sunnah zangu na Sunnah za makhaliyfah wangu waongofu na wenye kuongoza. Ziumeni kwa magego yenu. Na nakutahadharisheni na mambo yaliyozuliwa, kwani hakika kila kilichozuliwa ni Bid´ah.”[4]

[1] Salafiyyah sio kipote miongoni mwa mapote mengine kama ambavyo baadhi wanadhani na kudai hivo. Salafiyyah ni unasibisho wa Salaf na kushikamana barabara na mfumo wao, kama alivobainisha Shaykh (Hafidhwahu Allaah).  Kwa sababu Maswahabah walikuwa kama alivyowaeleza Ibn Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anhum):

“Yule anayetaka kuigiliza basi awaigilize wale waliokwishakufa. Kwa sababu aliye hai fitina haiaminiki juu yake. Hao ni Maswahabah wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambao walikuwa ndio watu bora kabisa. Nyoyo zao zilikuwa zikimcha Allaah zaidi, elimu yao ilikuwa imebobea na walikuwa wachache wa kujikalifisha. Allaah aliwachagua ili wasuhubiane na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na wasimamishe dini Yake. Hivyo zitambueni fadhilah zao na zifuateni athari zao. Kwani hakika wao walikuwa katika njia iliyonyooka.” (Jaamiy´ Bayaan-il-´Ilm wa Fadhwlih, uk. 419, na Mishkaat-ul-Maswaabiyh (193). Maneno ya Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) yako katika ”Hilyah” (1/305)) ya Abu Nu´aym.

Kamati ya kudumu ya utafiti na kutoa fatwa Saudi Arabia ilitoa fatwa ifuatayo:

”Salafiyyah ni unasibisho wa Salaf. Salaf ni Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), maimamu wa uongofu kutoka katika zile karne tau bora za kwanza (Radhiya Allaahu ´anhum). Salafiyyuun ni wingi wa ´Salafiy`. Ni wale wenye kufuata mfumo wa Salaf katika kufuata Qur-aan na Sunnah, kulingania katika vitu hivyo na kuvitendea kazi. Kwa hayo ndio wakawa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah.” (2/165)

[2] 09:100

[3] 59:10

[4] Abu Daawuud (4607), at-Tirmidhiy (2676) na Ibn Maajah (34). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”al-Irwaa’” (2455).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ajwibah al-Mufiydah ´an As-ilat-il-Manaahij al-Jadiydah, uk. 167-168
  • Imechapishwa: 26/06/2024
  • taaliki: Shaykh Jamaal bin Furahyaan al-Haarithiy