62. Mambo yaliyokatazwa ndani ya Ihraam

Imekatazwa kufanya mambo sita yafuatayo:

1 na 2 – Kunyoa nywele na kukata kucha. Kwa kunyoa nywele zisopungua tatu au kukata kucha zisopungua tatu, ni wajibu kutoa fidia ya kuchinja. Kwa kila nywele moja au kucha moja iliyo chini ya tatu, ni wajibu kutoa takriban gramu 510 ya chakula. Ikiwa nywele itaota ndani ya jicho lake akainyoa, nywele zake zikashuka na kufunika jicho lake akaziondoa au kucha yake ikavunjika akaikata, basi hana kinachomuwajibikia.

3 – Kuvaa nguo iliyoshonwa kwa ajili ya mwili. Isipokuwa ikiwa hatapata shuka ya chini, basi atavaa suruwali, ikiwa hatapata viatu, basi atavaa soksi za ngozi. Katika hali hiyo hana wajibu wa kutoa fidia.

4 – Kufunika kichwa ikiwa ni pamoja na masikio.

5 – Kujipulizia manukato katika mwili au nguo zake.

6 – Kuua mnyama wa kuwinda. Naye ni mnyama wa porini ambaye ni halali kuliwa. Ama mnyama wa kufugwa, si haramu kumuua. Kuhusu mnyama wa baharini, basi ni halali.

7 – Kufunga ndoa ni haramu. Hata hivyo hakuna fidia katika jambo hilo.

8 – Kumgusa mwanamke kwa matamanio bila kufanya tendo la ndoa katika sehemu ya siri. Ikiwa atatokwa na manii kwa sababu hiyo, ni wajibu kwake kuchinja ngamia. Ikiwa hatatokwa na manii, basi ni wajibu kwake kuchinja kondoo/mbuzi mmoja. Hajj yake ni sahihi.

9 – Kufanya tendo la ndoa ukeni. Ikiwa itakuwa kabla ya kutoka katika Ihraam kwa mara ya kwanza, basi Hajj yake itaharibika. Aidha ni wajibu kwake kuendelea na Hajj hiyo iliyoharibika na kufanya Hajj nyingine mwaka unaofuata. Vilevile ni wajibu kwa aliyefanya tendo la ndoa kuchinja ngamia.

Lakini ikiwa atafanya tendo la ndoa baada ya kutoka katika Ihraam kwa mara ya kwanza, basi ni wajibu kwake kuchinja kondoo/mbuzi mmoja na ataingia tena katika Ihraam kutoka Tan´iym ili afanye Twawaaf kwenye Ka´bah akiwa katika Ihraam.

Ikiwa atafanya tendo la ndoa katika ´Umrah, basi ´Umrah yake itaharibika.

´Ibaadah ya Hajj au ´Umrah haiharibiki kwa jambo jingine lolote katika mambo haya. Mwanamke ni kama mwanaume katika hukumu hizi, isipokuwa kwamba Ihraam yake ni katika uso wake na inaruhusiwa kwake kuvaa nguo iliyoshonwa.

  • Muhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy (afk. 620)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ´Umdat-ul-Fiqh, uk. 45-46
  • Imechapishwa: 09/11/2026