59 – Jaabir amesema:

”Wakati waliporejea Wahajiri wa bahari kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), akasema: ”Je, simweleze jambo la ajabu zaidi mliloona huko Uhabeshi?” Kijana mmoja kati yao akasema: ”Ee Mtume wa Allaah: ”Ee Mtume wa Allaah! Wakati tulipokuwa tumekaa alipita mmoja katika vikongwe wao. Alikuwa amebaba sufuria ya maji. Akapita karibu na kijana wao mmoja ambaye alimsukuma kwa nyuma, akaangukia magoti na hivyo sufuri yake ya maji ikapasuka. Alipoinuka, akageuka na kusema: ”Utajua, ee uliyeghurika, pindi Allaah atakapoweka Kursiy Yake, akawakusanya walimwengu wa mwanzo na wa mwisho na mikono na miguu ianze kusema vile ilivyokuwa wakivifanya. Utalijua jambo langu na jambo lako kesho mbele ya Allaah.” Ndipo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: ”Umesema kweli. Ni vipi Allaah atawatakasa watu ambao wanyonge wao hawachukui haki yao kutoka kwa wenye nguvu wao?”

Cheni ya wapokezi wake imesamilika[1].

[1] Ikiwa anakusudia kuwa ni njema kupitia zingine, maneno yake ni yenye kukubalika. La sivyo ameisimulia kupitia kwa Muslim bin Khaalid, kutoka kwa Ibn Khuthaym, kutoka kwa Abuz-Zubayr. Cheni hii ya wapokezi ni dhaifu kutokana naa sababu mbili. Mosi ni kwamba Abuz-Zubayr hataja wazi masimulizi yake. Alikuwa mfanya hadaa, jambo ambalo limetajwa na mtunzi mwenyewe katika ”Mizaan-ul-I´tidaal”. Pili ni kwamba Muslim bin Khaalid az-Zinjiyl ni dhaifu, kama ambavo mtunzi mwenyewe amelitaja na akanukuu maono ya maimamu juu yake. Wengi wao wanamdhoofisha kwa sababu ya kosa lake. Halafu akamalizia wasifu wake kwa maneno:

”Hadiyth hizi na mfano wake zinarudisha nguvu ya mtu na unyonge wake. Kupitia njia hii ameipokea Ibn Hibbaan (2584). Lakini Muslim hakupwekeka nayo katika kuisimulia. Ibn Maajah (4010) amesema:

“Sa´iyd bin Suwayda ametuhadithia: Yahyaa bin Sulaym ametuhadithia, kutoka kwa ´Abdullaah bin ´Uthmaan bin Khuthaym.”

Yahyaa na Sa´iyd wote wawili wana udhaifu pia, lakini hawana neno katika ufuatiliaji. Katika hali hii wamefuatiliwa na al-Fadhwl bin al-´Alaa´, ambaye amesimulia kuwa Ibn Khuthaym amemsimulia nayo. Imepokelewa na Ibn Hibbaan (1554) na al-Khatwiyb al-Baghdaadiy katika “Taariykh Baghdaad” (7/396).  Hadiyth kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) imesimuliwa kupitia kwa Jaabir na ipo katika “Shu´b-ul-Iymaan” (2/432/2). Inatiliwa nguvu pia na Abu Sa´iyd katika masimulizi mengine yaliyopo katika “Mishkaat-ul-Maswaabih” (3004). Katika “at-Targhiyb wat-Tarhiyb” (3/138) kuna nyingine inayoitia nguvu. Kwa al-Haakim (03/256) kuna nyingine tena inayoitia nguvu. Kwa msemo mwingine kunabakia ile kasoro ya kwanza, nayo ni kule Abuz-Zubayr kutotamka wazi masimulizi yake. Hata hivyo kisa hicho kimesimuliwa kupitia njia nyingine katika “al-Asmaa’ was-Swifaat”, uk. 404 na “Shu´b-ul-Iymaan” (2/432) ya al-Bayhaqiy, kutoka kwa ´Atwaa’ bin as-Saa-ib, kutoka kwa Muhaarib bin Dithaar, kutoka kwa Ibn Buraydah, kutoka kwa baba yake (Radhiya Allaahu ´anh), aliyesimulia:

”Wakati Ja´far alipofika kutoka Uhabeshi, Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimuuliza: ”Ni kitu gani cha kushangaza zaidi ulichokiona?” Akasema: ”Nimemuona mwanamke aliyebeba kikapu cha chakula kichwani, ambapo akapita karibu naye mpanda farasi na kukitupa. Akaketi chini na kuanza kukikusanya chakula chake. Kisha akamgeukia na kusema: ”Ole wako! Utafanyeje siku ambayo Mfalme ataweka Kursiy Yake na kuchukua kutoka kwa mwenye kudhuluma na kumpa aliyedhulumiwa?” Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akaanza kucheka na kustaajabishwa na maneno yake. Kisha akasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: ”Allaah asiutakase ummah ambao mnyonge hachukui haki yake kutoka mwenye nguvu yake.”

Hadiyth ingelikuwa ni Swahiyh kama sio kuchanganyikiwa kwa ´Atwaa´ bin as-Saa-ib. Hata hivyo inatumiwa kwa lengo la kutilia nguvu, na kwa hivyo Hadiyht ni njema – Allaah akitaka.

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Mukhtasar-ul-´Uluww, uk. 106-107
  • Imechapishwa: 26/06/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy