2 – ´Allaamah Ibn-ul-Qayyim (Rahimahu Allaah) amesema:
“Jibu hili la Maalik (Rahimahu Allaah) linatosha na ni lenye kuenea katika sifa zote. Ikiwa mtu kwa mfano atauliza kuhusiana na maneno Yake (Ta’ala):
إِنَّنِي مَعَكُمَا أَسْمَعُ وَأَرَىٰ
“Hakika Mimi Niko pamoja nanyi, Nasikia na Naona.”[1]
na akauliza namna anavyosikia na kuona, atajibiwa namna hiyohiyo: Kusikia na kuona kunajulikana. Namna haijulikani.
Vilevile ataambiwa yule mwenye kuuliza kuhusu Ujuzi, Uhai, Uwezo, Utashi, Ushukaji, Ghadhabu, Ridhaa, Neema, Kucheka na nyenginezo. Maana zao zote zinajulikana. Hata hivyo namna yake haieleweki. Kwa sababu ili mtu aweze kuelewa namna ni lazima kwanza aweze kuelewa Dhati na namna Ilivyo. Ikiwa hayo hayaeleweki kwa watu ni vipi basi wataelewa namna sifa Zake zilivyo?
Kinga yenye manufaa katika jambo hili ni kumsifu Allaah kwa yale aliyojisifu Mwenyewe na kwa yale aliyomsifu Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) – pasi na kupotosha, kukanusha, kumfanyia namna wala kumfananisha. Bali kinachokupasa ni kumthibitishia Yeye majina na sifa na umkanushie Yeye kufanana na viumbe. Namna hiyo makanusho yako yanakuwa yametakasika na mashabihisho na mathibitisho yako yametakasika na makanusho. Kwa hiyo yule anayepinga uhakika wa Kulingana juu ni mkanushaji, na yule mwenye kumlinganisha na kulingana kwa viumbe ni mfananishaj na mwenye kusema kwamba kulingana Kwake hakufanani na chochote kile ndiye mpwekeshaji mtakasaji.
Kanuni hiyohiyo ndiye yenye kutumika katika Kusikia, Kuona, Uhai, Matakwa, Uwezo, Mkono, Uso, Ridhaa, Ghadhabu, Kushuka, Kucheka na sifa nyinginezo zote ambazo amejieleza Mwenyewe.”[2]
[1] 20:46
[2] Madaarij-us-Saalikiyn (2/86).
- Muhusika: Shaykh ´Abdur-Razzaaq bin ´Allaamah ´Abdil-Muhsin al-´Abbaad al-Badr
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Athar al-Mash-huur ´an-il-Imaam Maalik fiy Swifat-il-Istiwaa’, uk. 83-84
- Imechapishwa: 17/12/2025
2 – ´Allaamah Ibn-ul-Qayyim (Rahimahu Allaah) amesema:
“Jibu hili la Maalik (Rahimahu Allaah) linatosha na ni lenye kuenea katika sifa zote. Ikiwa mtu kwa mfano atauliza kuhusiana na maneno Yake (Ta’ala):
إِنَّنِي مَعَكُمَا أَسْمَعُ وَأَرَىٰ
“Hakika Mimi Niko pamoja nanyi, Nasikia na Naona.”[1]
na akauliza namna anavyosikia na kuona, atajibiwa namna hiyohiyo: Kusikia na kuona kunajulikana. Namna haijulikani.
Vilevile ataambiwa yule mwenye kuuliza kuhusu Ujuzi, Uhai, Uwezo, Utashi, Ushukaji, Ghadhabu, Ridhaa, Neema, Kucheka na nyenginezo. Maana zao zote zinajulikana. Hata hivyo namna yake haieleweki. Kwa sababu ili mtu aweze kuelewa namna ni lazima kwanza aweze kuelewa Dhati na namna Ilivyo. Ikiwa hayo hayaeleweki kwa watu ni vipi basi wataelewa namna sifa Zake zilivyo?
Kinga yenye manufaa katika jambo hili ni kumsifu Allaah kwa yale aliyojisifu Mwenyewe na kwa yale aliyomsifu Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) – pasi na kupotosha, kukanusha, kumfanyia namna wala kumfananisha. Bali kinachokupasa ni kumthibitishia Yeye majina na sifa na umkanushie Yeye kufanana na viumbe. Namna hiyo makanusho yako yanakuwa yametakasika na mashabihisho na mathibitisho yako yametakasika na makanusho. Kwa hiyo yule anayepinga uhakika wa Kulingana juu ni mkanushaji, na yule mwenye kumlinganisha na kulingana kwa viumbe ni mfananishaj na mwenye kusema kwamba kulingana Kwake hakufanani na chochote kile ndiye mpwekeshaji mtakasaji.
Kanuni hiyohiyo ndiye yenye kutumika katika Kusikia, Kuona, Uhai, Matakwa, Uwezo, Mkono, Uso, Ridhaa, Ghadhabu, Kushuka, Kucheka na sifa nyinginezo zote ambazo amejieleza Mwenyewe.”[2]
[1] 20:46
[2] Madaarij-us-Saalikiyn (2/86).
Muhusika: Shaykh ´Abdur-Razzaaq bin ´Allaamah ´Abdil-Muhsin al-´Abbaad al-Badr
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Athar al-Mash-huur ´an-il-Imaam Maalik fiy Swifat-il-Istiwaa’, uk. 83-84
Imechapishwa: 17/12/2025
https://firqatunnajia.com/62-jibu-kama-alivyojibu-maalik/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket