149 – Anas (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Asitamani mmoja wenu kifo kwa sababu ya dhara lililompata. Ikiwa hana budi, basi aseme:
اللَّهُمَّ أَحْيِنِي مَا كَانَتْ الْحَيَاةُ خَيْرًا لِي، وَتَوَفَّنِي إِذَا كَانَتْ الْوَفَاةُ خَيْرًا لِي
“Ee Allaah! Nibakize kuwa hai ikiwa uhai ni kheri kwangu na nifishe ikiwa kufa ni kheri kwangu.”[1]
Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.
Imekuja katika tamko jengine:
“Asitamani mmoja wenu kifo. Kwani hakika umri wa muumini haumzidishii isipokuwa kheri.”[2]
MAELEZO
Muumini hatamani kifo kwa sababu ya msiba uliyompata katika mwili au nafsi yake. Bali ni lazima kwake kusubiri. Hilo ni kwa sababu mtu hajui ni kipi kinachofuata baada ya kufa. Jengine ni kwamba umri wa muumini haumzidishii isipokuwa kheri. Hata hivyo hapana vibaya akichelea kupatwa na mtihani katika dini. Jambo hilo limefanywa na kikosi cha Salaf wakati walipochelea kupatwa na mtihani katika dini. Sahihi zaidi ni kwamba ajaalie kheri kwa Allaah (´Azza wa Jall), kama ilivyofahamisha Hadiyth.
[1] al-Bukhaariy (6351) na Muslim (2680).
[2] Muslim (2682).
- Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 141
- Imechapishwa: 15/11/2025
149 – Anas (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Asitamani mmoja wenu kifo kwa sababu ya dhara lililompata. Ikiwa hana budi, basi aseme:
اللَّهُمَّ أَحْيِنِي مَا كَانَتْ الْحَيَاةُ خَيْرًا لِي، وَتَوَفَّنِي إِذَا كَانَتْ الْوَفَاةُ خَيْرًا لِي
“Ee Allaah! Nibakize kuwa hai ikiwa uhai ni kheri kwangu na nifishe ikiwa kufa ni kheri kwangu.”[1]
Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.
Imekuja katika tamko jengine:
“Asitamani mmoja wenu kifo. Kwani hakika umri wa muumini haumzidishii isipokuwa kheri.”[2]
MAELEZO
Muumini hatamani kifo kwa sababu ya msiba uliyompata katika mwili au nafsi yake. Bali ni lazima kwake kusubiri. Hilo ni kwa sababu mtu hajui ni kipi kinachofuata baada ya kufa. Jengine ni kwamba umri wa muumini haumzidishii isipokuwa kheri. Hata hivyo hapana vibaya akichelea kupatwa na mtihani katika dini. Jambo hilo limefanywa na kikosi cha Salaf wakati walipochelea kupatwa na mtihani katika dini. Sahihi zaidi ni kwamba ajaalie kheri kwa Allaah (´Azza wa Jall), kama ilivyofahamisha Hadiyth.
[1] al-Bukhaariy (6351) na Muslim (2680).
[2] Muslim (2682).
Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 141
Imechapishwa: 15/11/2025
https://firqatunnajia.com/62-duaa-wakati-mtu-amekata-tamaa-ya-kuendelea-kueshi/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket