Fahamu ya kwamba majuto yote ni kujishughulisha na yule ambaye kukushughulisha naye hakuzai chochote isipokuwa kupoteza sehemu yako na fungu lako mbele ya Allaah (´Azza wa Jall), kukukatisha kutokana Naye, kupoteza muda wako, kudhoofisha azma yako na kutawanya fikira zako. Ukipewa mtihani naye, jambo ambalo haliepukiki, basi fanya matendo kwa ajili ya Allaah (´Azza wa Jall) katika jambo hilo, utaraji malipo kwa Allaah kwa ajili yake kwa kadiri uwezavyo, jikurubishe kwa Allaah kwa yale yanayomridhisha na ufanye kukutana naye kuwa ni biashara kwako na wala usikufanye kuwa ni khasara kwako. Uwe naye kama mtu anayetembea barabarani kisha akakutana na mtu akamzuia asiendelee na safari yake. Jitahidi umchukue uende naye na umsukume aende wala yeye asikushike. Akikataa na haionekani matumaini ya yeye kutembea, basi usisimame naye na shika njia yako na muache. Usimgeukie kwa sababu huyo ni mkataji wa njia, pasi na kujali ni nani. Basi okoa moyo wako. Uthamini mchana na usiku wako. Jua lisikuzamie kabla hujafikia kituo ambapo ukachukuliwa au alfajiri kuchomoza na ukawa bado hujafika. Utawezaje kukutana nao?
- Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 112
- Imechapishwa: 21/08/2025
Fahamu ya kwamba majuto yote ni kujishughulisha na yule ambaye kukushughulisha naye hakuzai chochote isipokuwa kupoteza sehemu yako na fungu lako mbele ya Allaah (´Azza wa Jall), kukukatisha kutokana Naye, kupoteza muda wako, kudhoofisha azma yako na kutawanya fikira zako. Ukipewa mtihani naye, jambo ambalo haliepukiki, basi fanya matendo kwa ajili ya Allaah (´Azza wa Jall) katika jambo hilo, utaraji malipo kwa Allaah kwa ajili yake kwa kadiri uwezavyo, jikurubishe kwa Allaah kwa yale yanayomridhisha na ufanye kukutana naye kuwa ni biashara kwako na wala usikufanye kuwa ni khasara kwako. Uwe naye kama mtu anayetembea barabarani kisha akakutana na mtu akamzuia asiendelee na safari yake. Jitahidi umchukue uende naye na umsukume aende wala yeye asikushike. Akikataa na haionekani matumaini ya yeye kutembea, basi usisimame naye na shika njia yako na muache. Usimgeukie kwa sababu huyo ni mkataji wa njia, pasi na kujali ni nani. Basi okoa moyo wako. Uthamini mchana na usiku wako. Jua lisikuzamie kabla hujafikia kituo ambapo ukachukuliwa au alfajiri kuchomoza na ukawa bado hujafika. Utawezaje kukutana nao?
Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 112
Imechapishwa: 21/08/2025
https://firqatunnajia.com/61-jihadhari-na-vikengeusha-fikira-vyako/