148 – ´Abdullaah bin Abiy Awfaa (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia: “Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliomba siku ya Ahzaab dhidi ya washirikina akasema:

اللَّهُمَّ مُنْزِلَ الكِتَابِ، سَرِيعَ الحِسَابِ، اللَّهُمَّ اهْزِمِ الأَحْزَابَ اللَّهُمَّ اهْزِمْهُمْ وَزَلْزِلْهُمْ

”Ee Allaah! Mteremsha wa Kitabu, mfanya haraka kuhesabu. Ee Allaah! Vishinde vikosi. Ee Allaah! Washinde na watetemeshe.”[1]

Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.

MAELEZO

Hadiyth hii ndani yake kuna kuomba du´aa dhidi ya washirikina wakati wamekusanyika vikundi, kukandamiza na kudhuru. Kwa hiyo ni lazima kwa kila muislamu kumuomba Allaah (´Azza wa Jall) kwa mfano wa du´aa hii awatetemeshe washirikina na makundi yale ambayo yalikusanyika dhidi ya waislamu. Aidha aingize khofu ndani ya nyoyo zao, asambaratishe umoja wao, awaparanganishe na akate mizizi yao na atutosheleze sisi na waislamu wengine kutokana na shari yao.

[1] al-Bukhaariy (2933) na Muslim (1742).

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 140
  • Imechapishwa: 15/11/2025