Kituo cha watu wa Madiynah ni Dhul-Hulayfah.

Kituo cha watu wa Shaam, watu wa magharibi na misri ni Juhfah.

Kituo cha Yemen ni Yalamlam.

Kituo cha Najd ni Qarn.

Kituo cha watu wa mashariki ni Dhaat ´Irq.

Hivi ni vituo vyao na vya kila anayepita hapo. Yule mwenye makazi yake yako karibu zaidi na kituo kuliko kituo hicho, basi kituo chake ni kutoka katika makazi yake. Hata watu wa Makkah wanaingia katika Ihraam kutoka huko kwa ajili ya Hajj yao, na wanaingia katika Ihraam kwa ajili ya ´Umrah kutoka sehemu iliyo karibu zaidi nje ya mipaka ya Haram. Yule mwenye njia yake haipiti katika kituo chochote, basi kituo chake ni sambamba na kituo kilicho karibu zaidi naye.

Haijuzu kwa mwenye kutaka kuingia Makkah kupita kituo bila kuwa katika Ihraam, isipokuwa kwa ajili ya mapambano yanayoruhusiwa au kwa haja inayojirudia mara kwa mara kama mkata kuni na mfano wake. Kisha akitaka kufanya ´ibaadah ya Hajj au ´Umrah, ataingia katika Ihraam kutoka mahali alipo.

Ikiwa atapita kituo bila kuwa katika Ihraam, atarudi na kuingia katika Ihraam kutoka kituoni, na si wajibu kwake kuchinja fidia. Kwa sababu ameingia katika Ihraam kutoka katika kituo chake. Lakini ikiwa ataingia katika Ihraam kabla ya kituo, basi ni wajibu kwake kutoa fidia, ni mamoja ikiwa atarudi kituoni au asirudi.

Bora ni kutoingia katika Ihraam kabla ya kituo. Lakini akifanya hivyo, anakuwa ndani ya Ihraam.

Miezi ya Hajj ni Shawwaal, Dhul-Qa´dah na siku kumi za Dhul-Hijjah.

  • Muhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy (afk. 620)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ´Umdat-ul-Fiqh, uk. 45
  • Imechapishwa: 05/11/2026