227 – Hudbah ametuhadithia: Hammaad bin Salamah ametukhabarisha, kutoka kwa Thaabit, kutoka kwa Anas, ambaye amesema:

“’Adhwbaa’ kamwe hatangulizi mbele kwa mbio. Siku bedui mmoja akaja na ngamia wake, au punda wake, na kutaka kumpita na kumshinda. Ni kama kwamba jambo hilo lilikuwa zito kwa Maswahabah wa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam), ndipo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) akasema: “Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) hajafanya kamwe kunyanyua kitu chochote cha duniani isipokuwa pia baadaye hukishusha.”[1]

[1] al-Bukhaariy (6501).

  • Muhusika: Imaam Abu Bakr Ahmad bin Abiy ´Aaswim ash-Shaybaaniy (a.f.k. 287)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-uz-Zuhd, uk. 60-61
  • Imechapishwa: 21/07/2025