6 – Waziri wa mambo ya nje an-Nuqraashiy aliuawa na Khawaarij

Ulimwengu wa Kiislamu na wa kiarabu na bali mpaka mabara mengi yametishwa kwa kuuawa kwa mwanaume wa shoka, naye ni shahidi an-Nuqraashiy[1]. Allaah amsamehe na amkutanishe na wakweli, mashahidi na waja wema.

Hapo kabla kulijitokeza ajali nyingi. Baadhi yazo zilipelekwa mahakamani na akazungumza alozungunza. Lengo langu sasa ni kukosoa mahakama. Mimi nilisoma jarima za siasa kama wengine. Hujiuliza mwenyewe kama tunaishi katika mji ulio na waislamu.

Ninaonelea kuwa ni wajibu kwangu kubainisha jambo hili kwa njia sahihi ya Kishari´ah ili kusiwepo udhuru kwa yeyote. Huenda Allaah akawaongoza baadhi kutoka kwenye jarima hizi za ki-Khawaarij na wakarejea katika dini yao kabla mambo hayajachelewa. Sijui ni nani watu hawa wamepangilia kumuua baada ya an-Nuqraashiy…

Katika Aayah nyingi Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) ametishia vikali kuiua nafsi iliyoharamishwa:

وَمَن يَقْتُلْ مُؤْمِنًا مُّتَعَمِّدًا فَجَزَاؤُهُ جَهَنَّمُ خَالِدًا فِيهَا وَغَضِبَ اللَّـهُ عَلَيْهِ وَلَعَنَهُ وَأَعَدَّ لَهُ عَذَابًا عَظِيمًا

“Na atakayemuua muumini kwa kusudi, basi jazaa yake ni [Moto wa] Jahannam, atawekwa humo kwa muda mrefu na Allaah atamghadhibikia na atamlaani na atamuandalia adhabu kuu.” (04:93)

Haya ni katika mambo ya Uislamu yaliyo wazi. Mjinga anayajua kabla ya msomi. Aayah inahusiana na mauaji ya kukusudia yanayopitika kati ya watu wakati wa matukio, wizi na mfano wa hayo ambapo muuaji anaua na huku anajua kuwa anatenda dhambi kubwa.

Ama kuhusiana na mauaji ya kisiasa ambayo tumesikia majadiliano marefu juu yake, hilo ni suala lingine kabisa na kitu kingine.

Pindi muuaji wa siasa anapoua hujihisi utulivu ndani ya nafsi na mwenye kuridhia. Anaamini kuwa tendo lake ni jema. Kutokana na propaganda batili anaamini kuwa anafanya kitu ambacho ni halali na kinachojuzu. Pengine akafikia mpaka kuonelea kuwa amefanya wajibu wa Kiislamu ambao wengine wameupuuzia. Mtu kama huyu ni mwenye kuritadi na kutoka katika Uislamu. Ni wajibu kutangamana naye matangamano kama ya wenye kuritadi na kuhukumiwa hukumu ya Kishari´ah na kanuni.

Ni Khawaarij kama wale Khawaarij wa zamani ambao walikuwa wakiwapiga vita Maswahabah wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kuwasalimisha washirikina wenye kukiri kuwa ni makafiri. Walikuwa kama Khawaarij wa leo. Bali wao walikuwa ni bora. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwaeleza kwa Wahyi kabla hata ya kuwaona. Aliwaambia Maswahabah zake:

“Mtazidharau swalah zenu na za kwao na swawm zenu na swawm zao. Wanasoma Qur-aan na haivuki kwenye shingo zao. Wanatoka katika Uislamu kama jinsi mshale unavotoka kwenye upinde wake.”[2]

Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) tena:

“Katika kipindi cha mwisho kutajitokeza watu wenye meno madogo na wapumbavu wa akili. Wanazungumza kwa maneno ya kiumbe mbora kabisa na wanasoma Qur-aan pasina kuvuka shingo zao. Wanatoka katika dini kama jinsi mshale unavotoka kwenye upinde wake. Mkikutana nao waueni. Yule mwenye kuwaua ana ujira mbele ya Allaah siku ya Qiyaamah[3].”[4]

Hadiyth zenye maana kama hii ni nyingi na zimepokelewa kupitia wapokezi wengi kutoka kila pande. Ni katika mambo ya Uislamu yaliyo wazi. Zinasema ya kwamba yule mwenye kuonelea kuwa ni halali kumwaga damu iliyoharamishwa basi amejivua mtego wa Uislamu kutoka shingoni mwake. Hii ndio hukumu ya mauaji ya kisiasa. Ni mabaya zaidi kuliko mauaji ya kukusudia yanayopitika kati ya watu. Mauaji kama haya Allaah anaweza akayasamehe kwa fadhila na huruma Wake na Anaweza vilevile kufanya adhabu yake ikawa kafara kwa dhambi yake. Mauaji haya sio kama mauaji ya kisiasa ambayo muuaji anaendelea kushikamana na fikira yake katika kuua, anajisifu kwayo na kwamba ni juhudi za kishujaa.

Kuna Hadiyth nyingine juu ya mauaji ya kisiasa ambayo hakuna namna ya kuweza kuifasiri kimakosa. Kulikuwa utata wa kisiasa kati ya az-Zubayr bin al-´Awaam na ´Aliy bin Abiy Twaalib ambao mwisho wake iliku vita vya ngamia. Mtu alikuja kwa az-Zubayr na kumwambia:

“Nimuue ´Aliy kwa ajili yako?” Akasema: “Hapana. Vipi basi utamuua ilihali yuko na wanajeshi pamoja naye?” Akasema: “Ninajiunga naye na kumuua mauaji ya uficho.” Ndipo az-Zubayr akasema: “Hapana. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema: “Imani inadhibiti mauaji. Muumini haui.”[5]

Bi maana imani inamzuia muumini kutotumbukia kwenye kuritadi. Mwenye kuua hawi muumini.

Ama kuhusu an-Nuqraashiy Allaah amemkirimu shahada. Anapata fadhila na utukufu wa mashahidi mbele ya Allaah. Amekufa kifo ambacho Maswahabah wengi wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) walikuwa wakikitamani. ´Umar bin al-Khattwaab alikitamani na akakipata na akawa ni mwemye kufikia nafasi kubwa na ngazi ya juu mbele ya Allaah.

Dhambi, fedheha na makemeo yasiwe juu ya mwingine isipokuwa hawa Khawaarij wauaji wenye kuhalalisha kumwaga damu iliyoharamishwa na wale wenye kuwatetea na wanataka kuitupa nchi yetu (Misri) kwenye dinbwi kama la Ulaya. Haya ndio malengo yao kuhalalisha mauaji ya kisiasa na kukhafifisha adhabu yake. Hawajui kile wanachokifanya. Sitaki kuwatuhumu kuwa wanajua na wanataka.

Usaamah bin Ahmad Shaakir (Rahimahu Allaah) amesema:

“Baada ya makala hii kuenea waziri wa mambo ya ndani akapata khabari kuwa kuna mpango wa kumuua Shaykh Ahmad Muhammad Shaakir. Kukawekwa polisi wanaume kuilinda nyumba yake. Hata hivyo Shaykh akaomba nyumba yake isilindwe kutokana na matatizo yanayosababishwa na jambo hilo. Tatizo kubwa ilikuwa pindi waziri wa mambo ya ndani wa sasa Saudi Arabia mtoto wa mfalme Naayif bin ´Abdil-´Aziyz Aal as-Su´uud alipokuja kumtembelea Shaykh Ahmad Muhammad Shaakir nyumbani kwake ´Abbaasiyyah. Walinzi wakamzuia asipande juu. Ndipo nikawa nimemteremkia na kumtaka udhuru na kumwita apande kwa baba. Baada ya hapo ndipo walinzi wakaondoshwa nyumbani kwetu.”[6]

[1] Tazama http://en.wikipedia.org/wiki/Mahmoud_an-Nukrashi_Pasha

[2] Muslim (01/292).

[3] Tazama https://firqatunnajia.com/nani-mwenye-haki-ya-kuwaua-khawaarij__trashed/

[4] Muslim (1/293).

[5] Ahmad (1429).

[6] Min A´laam-il-Aswr, uk. 51.

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad Shaakir
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Gazeti al-Asaas 1949-01-02 Lamahaat ´an Da´wat-il-Ikhwaan al-Muslimiyn, uk. 19-22
  • mkusanyaji: Muhammad bin ´Iwadhw bin ´Abdil-Ghaniy