Sunnah Swahiyh inafahanmisha ukaribu wa Allaah kwenye moyo unaonyenyekea mitihani Yake, unaokuwa na subira juu ya mipango Yake au kuiridhia. Muslim amepokea kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ambaye amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah (´Azza wa Jall) atasema siku ya Qiyaamah: “Ee mwanadamu! Niliumwa na hukunitembelea.” Atasema: ”Ee Mola, nitakutembeleaje na hali Wewe ni Mola wa walimwengu wote?” Ndipo atasema: “Je, hukujua kuwa mja Wangu fulani alikuwa mgonjwa na hukumtembelea? Je, hukujua kwamba kama ungemtembelea, basi ungenikuta Kwake?”[1]

Abu Nu´aym amepokea kupitia kwa Hamzah, kutoka kwa Ibn Shawdhab ambaye amesema:

“Allaah (Ta’ala) aliteremsha wahy kwa Muusa: “Hivi unajua ni kwa nini Nimekuteuwa juu ya watu wote kwa Ujumbe na maneno Yangu?” Akasema: ”Hapana, ee Mola.” Akasema: “Kwa sababu hakuna yeyote ambaye alininyenyekea kama ulivyoninyenyekea Wewe.”[2]

Unyenyekevu ni unyenyekevu wenye manufaa na ndio kitu cha kwanza kinachotolewa na elimu.

[1] Muslim (2569).

[2] Hilyat-ul-Awliyaa’ (6/130).

  • Muhusika: Imaam Zayn-ud-Diyn ´Abdur-Rahmaan bin Rajab al-Hanbaliy (afk. 795)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Khushuu´ fiys-Swalaah, uk. 41-43
  • Imechapishwa: 24/11/2025