59. Usidanganyike na waganga wenye kuitwa Mashaykh, waalimu na maustadhi

Miongoni mwa mambo ambayo ni lazima kuyazindua na watu wazindukane nayo ni kwamba wachawi, makuhani na wapiga ramli wanacheza na ´Aqiydah za watu kwa njia ya kujidhihirisha kwa muonekano wa matabibu. Kisha wanawaamrisha wagonjwa kuchinja kwa ajili ya asiyekuwa Allaah na kwamba wachinje kondoo au kuku yenye sifa hii na ile, wanawaandikia talasimu za kishirki na utakaji ulinzi wa ki-Shaytwaan kwa sifa ya hirizi wanazowavalisha shingoni mwao, wanaziweka kwenye masanduku yao au katika nyumba zao.

Baadhi ya wengine wanajidhihirisha kwa muonekano wa kuelezea mambo yaliyofichikana na vilipo vitu vilivyopotea kwa njia ya kwamba anakuja mtu mjinga na kumuuliza ni wapi vipo vitu vilivyopotea na baadaye wakawaeleza au wakawaletea navyo kwa msaada wa watumishi wao katika mashaytwaan.

Wengine wanajidhihirisha kwa muonekano wa walii ambaye yuko na makarama au kwa muonekano wa mwanasanaa kama vile kuingia ndani ya moto na usimuathiri kitu, kujidunga kisu, kujilaza chini ya magurudumu ya magari  na hayamuathiri kitu au mengineyo katika mambo ya kiganga ambayo ukweli wa mambo ni uchawi ambao ni katika matendo ya shaytwaan. Mambo hayo yanapitika kupitia kwa watu hawa kwa sababu ya majaribio au ni mambo ya kiinimacho yasiyokuwa na ukweli wowote. Bali ni hila zilizojificha wanazozifanya mbele ya macho, kama walivofanya wachawi wa Fir´awn kwa vitu kama kambakamba na mabakora. Shaykh-ul-Islaam amesema, wakati alipokuwa akijadiliana na wachawi Batwaaihiyyah Ahmadiyyah ar-Rifaa´iyyah, Shaykh wa Batwaaihiyyah alisema hali ya kunyanyua sauti yake: “Sisi tuna hali fulani na fulani na akadai hali zisizokuwa za kawaida kama vile za moto, nyenginezo na kwamba hali hizo wanasifika nazo wao tu na kwamba hali inastahiki kujisalimisha kwao kwa ajili yake.” Shaykh-ul-Islaam akasema:

“Nikasema, hali ya kunyanyua sauti yangu na nikaghadhibika: “Mimi namsemeza kila ambaye ni Ahmadiy, kuanzia mashariki mwa ulimwengu mpaka magharibini kwake, ni kitu gani alichofanya ndani ya moto? Mimi nafanya mfano wa kile mnachofanya na ambaye ataungua basi huyo ameshindwa. Pengine hata nilisema: “Basi huyo atakuwa na laana za Allaah.” Lakini hayo yatafanyika baada ya kuiosha miili yetu kwa siki na kwa maji ya moto. Viongozi na watu wakaniuliza kuhusu hilo ambapo nikasema: “Watu hawa wana ujanja wakati wa kuwasiliana na moto wanaufanya kwa vitu katika mafuta ya vyura, maganda ya machungwa na mawe. Wakafedheka mbele ya watu kwa sababu hiyo.”[1]

Malengo yake ni kuweka wazi kuwa watu hawa waongo huwadanganya watu kwa mfano ujanja kama huu uliojificha kama mfano wa kuivuta gari kwa unywele, kujilaza chini ya magurudumu yake, kujidunga mshikaki wa chuma machoni mwake na mengineyo katika mambo ya kichawi ya kishaytwaan.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (11/464-466).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ´Aqiydat-ut-Tawhiyd, uk. 107-109
  • Imechapishwa: 23/03/2020