59. Mazungumzo ya Mtume na Maswahabah zake kuhusu ulimwengu

224 – Abur-Rabiy´ az-Zahraaniy ametuhadithia: ´Abdullaah bin Yaziyd al-Muqri’ ametukhabarisha: al-Layth bin Sa´d ametukhabarisha, kutoka kwa al-Waliyd bin Abiyl-Waliyd, kutoka kwa Sulaymaan bin Khaarijah bin Zayd bin Thaabit, kutoka kwa baba yake, ambaye amesema:

”Kikundi cha watu kiliingia kwa Zayd bin Tthaabit na kusema: “Tuambie kuhusu Mtume wa  Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam)!” Akasema: “Nilikuwa jirani yake. Ilikuwa tunapozungumza kuhusu Aakhirah, basi anafanya vivyo hivyo na sisi. Na wakati tukitaja dunia, basi anafanya vivyo hivyo na sisi.”[1]

225 – Ibn Hisaab ametukhabarisha: Hammaad bin Zayd ametukhabarisha, kutoka kwa Yahyaa bin Sa´iyd, kutoka kwa ´Umar bin Kathiyr bin Aflah, kutoka kwa ´Ubayd Sanuutwaa, kutoka kwa Khawlah bint Qays bin Qahd, ambaye alikuwa mke wa Hamzah, ambaye amesema:

“Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) alikuja kwa Hamzah, ambapo wakazungumza kuhusu dunia.”[2]

226 – Ibn Waarah ametuhadithia: Muhammad bin Sa´iyd bin Saabiq ametukhabarisha: ´Amr bin Abiy Qays ametukhabarisha, kutoka kwa Ibraahiym bin al-Muhaajir, kutoka kwa Qays bin Abiy Haazim, kutoka kwa al-Mustawrid, ambaye amesimulia:

“Nilipokuwa kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam)  tulizungumza kuhusu duniani, ambapo akasema: “Hayakuwa maisha ya dunia ukilinganisha na Aakhirah isipokuwa ni kama ambavo mmoja wenu anavyochovya kidole chake baharini kisha atazame atarudi na kitu gani.”[3]

[1] Dhaifu kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Mukhtaswar-ush-Shamaa-il al-Muhammadiyyah” (294).

[2] Ahmad (26515).

[3] Muslim (2858).

  • Muhusika: Imaam Abu Bakr Ahmad bin Abiy ´Aaswim ash-Shaybaaniy (a.f.k. 287)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-uz-Zuhd, uk. 59-60
  • Imechapishwa: 21/07/2025