59. Du´aa wakati wa kumswalia maiti swalah ya jeneza

145 – ´Awf bin Maalik al-Ashja´iy (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia: “Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimswalia maiti ambapo nikahifadhi kutoka katika du´aa yake akisema:

اللهُمَّ اغْفِرْ لَهُ وَارْحَمْهُ وَعَافِهِ وَاعْفُ عَنْهُ، وَأَكْرِمْ نُزُلَهُ، وَوَسِّعْ مُدْخَلَهُ، وَاغْسِلْهُ بِالْمَاءِ وَالثَّلْجِ وَالْبَرَدِ، وَنَقْهِ مِنَ الْخَطَايَا كَمَا نَقَيْتَ الثَّوْبَ الْأَبْيَضَ مِنَ الدَّنَسِ، وَأَبْدِلْهُ دَارًا. خَيْرًا مِنْ دَارِهِ، وَأَهْلًا خَيْرًا مِنْ أَهْلِهِ وَزَوْجًا خَيْرًا مِنْ زَوْجِهِ، وَأَدْخِلْهُ الْجَنَّةَ وَأَعِذْهُ مِنْ عَذَابِ الْقَبْرِ – أَوْ مِنْ عَذَابِ النَّارِ

“Eee Allaah! Mghufurie na mrehemu, muafu na msamehe na mtukuze kushuka kwake [kaburini] na mpanulie maingilio yake na muoshe na maji na kwa theluji na barafu na mtakase na makosa kama Ulivyoitakasa nguo nyeupe kutokamana na uchafu na mbadilishie nyumba bora kuliko nyumba yake na jamaa bora kuliko jamaa zake na mume bora kuliko mke wake na mwingize Pepo na mlinde na adhabu ya kaburi na adhabu ya kaburi – au na adhabu ya Moto.”[1]

Ameipokea Muslim.

MAELEZO

Katika Hadiyth hii kuna ya kwamba inapendeza kwa muislamu kumuombea maiti wakati wa kumswalia swalah ya jeneza du´aa hii.

Maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“… na mume bora kuliko mke wake… ”

Ikiwa maiti ni mwanaume. Hakusemwi namna hii ikiwa maiti ni mwanamke. Badala yake mtu atasema:

جوارا خيرا من جوارها

“… jirani bora kuliko jirani yake.”

[1] Muslim (963).

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 138
  • Imechapishwa: 15/11/2025