220 – Ibn Numayr ametukhabarisha: Abu Mu´aawiyah ametukhabarisha, kutoka kwa al-A´mash, kutoka kwa Abu Swaalih, kutoka kwa Abu Sa´iyd, ambaye amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema kuhusiana na maneno Yake (Ta´ala):
وَأَنذِرْهُمْ يَوْمَ الْحَسْرَةِ إِذْ قُضِيَ الْأَمْرُ وَهُمْ فِي غَفْلَةٍ
“Waonye Siku ya majuto itakapohukumiwa amri na hali wao wamo katika ghafla…”[1]
”Kwa maana duniani.”
221 – Muhammad bin ´Ubayd bin Hisaab ametuhadithia: Muhammad bin Thawr ametukhabarisha, kutoka kwa Ma´mar, kutoka kwa az-Zuhriy, kutoka kwa ´Ubaydullaah bin Abiy Thawr, kutoka kwa Ibn ´Abbaas, kutoka kwa ´Umar bin al-Khattwaab, ambaye ameeleza kuwa amesema:
“Ee Mtume wa Allaah! Muombe Allaah autajirishe ummah wako. Amewatajirisha Wafursi na Warumi ambao hata hawamwabudu Allaah.” Akaketi na kusema: “Je, una shaka na mimi, ee mwana wa al-Khattwaab? Hao ni watu ambao yameharakishwa mazuri yao katika maisha yao ya dunia.”[2]
222 – Abu Bakr ametukhabarisha: Ghundar ametukhabarisha, kutoka kwa Shu´bah, kutoka kwa Daawuud bin Faraahiyj: Nimemsikia Abu Hurayrah akisema:
“Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) aliwahama wakeze (nadhani kuwa alisema hivo), ndipo ´Umar bin al-Khattwaab akaingia kwake. Alikuwa chumbani kwake kwenye mkeka wa majani, ambao ulikuwa umemtia alama mgongoni mwake. Akasema: “Ee Mtume wa Allaah! Kisraa anakunywa kutoka kwenye dhahabu na fedha na wewe unakunywa namna hii?” Ndipo Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) akasema: “Hakika wao wameharakishiwa mazuri yao katika maisha ya dunia.”[3]
223 – Kaamil bin Twalhah ametuhadithia: Mubaarak bin Fadhwaalah ametukhabarisha, kutoka kwa al-Hasan, kutoka kwa Anas bin Maalik, ambaye amesema:
“Niliingia kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam), ambaye alikuwa amelala juu ya kitanda kilichofumwa kwa utepe. Hakukuwa na karatasi kati ya ngozi yake na vifungo. Chini ya kichwa chake alikuwa na mto wa ngozi uliojazwa nyuzi za makuti. Maswahabah kadhaa walimtembelea, lakini ´Umar alipoingia aliona jinsi bendi zilivyokuwa zimemtia alama kwenye ubavu wake na akabubujikwa na machozi. Akasema: “Kwa nini unalia?” Akasema: “Naapa kwa Allaah! Silii isipokuwa ni kwa sababu najua kuwa wewe ndiye mtukufu zaidi mbele ya Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) kuliko Kisraa na Kayswar, ambao wanaishi kama wanavyoishi duniani.” Ndipo Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) akasema: “Je, huridhii wao kuwa na dunia na sisi tukawa na Aakhirah?”[4]
[1]19:39
[2] al-Bukhaariy (2468) na Muslim (1479).
[3] Ahmad (7903).
[4] Ahmad (12009).
- Muhusika: Imaam Abu Bakr Ahmad bin Abiy ´Aaswim ash-Shaybaaniy (a.f.k. 287)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Kitaab-uz-Zuhd, uk. 58-59
- Imechapishwa: 20/07/2025
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket