58. Watu sampuli saba kwenye kivuli cha Allaah

55 – Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ameelea kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Watu sampuli saba Allaah atawaweka kwenye kivuli Chake siku ambayo hakuna kivuli isipokuwa Chake; kiongozi mwadilifu, kijana ambaye amekulia katika kumwabudu Allaah, mtu ambaye moyo wake umefungamana na misikiti, wanaume wawili wamependana kwa ajili ya Allaah ambapo wamekusanyika kwa ajili Yake na wakaachana kwa ajili Yake, mwanaume ambaye ameitwa na mwanamke aliye na nafasi na mzuri ambapo akasema “Mimi namuogopa Allaah, Mola wa walimwengu”, mtu ambaye ametoa swadaqah akaificha hadi mkono wake wa kushoto usijue kilichotolewa na mkono wake wa kushoto na mtu ambaye amemkumbuka Allaah akiwa peke yake macho yake yakabubujika machozi.”[1]

Ameipokea al-Bukhaariy[2].

[1] al-Bukhaariy (660) na Muslim (1031).

[2] Ameipokea pia Muslim, Ahmad na wengineo. Imetajwa katika “Irwaa’-ul-Ghaliyl” (887).

  • Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Mukhtasar-ul-´Uluww, uk. 105
  • Imechapishwa: 26/06/2024
  • Taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy