Maana yake ni kulazimiana na msikiti kwa ajili ya kumtii Allaah (Ta´ala) ndani yake. Hiyo ni Sunnah, isipokuwa ikiwa ni nadhiri, basi inawajibika kuitimiza.
Ni sahihi kwa mwanamke kufanya I´tikaaf katika kila msikiti isipokuwa mahali pa kuswalia nyumbani kwake. Si sahihi kwa mwanaume kukaa I´tikaaf isipokuwa ndani ya msikiti ambao kunaswaliwa swalah ya mkusanyiko. I´tikaaf yake katika msikiti ambao kunaswaliwa swalah ya ijumaa ndio bora.
Yule mwenye kuweka nadhiri ya kufanya I´tikaaf au kuswali katika msikiti fulani, basi inaruhusiwa kwake kufanya hivyo katika msikiti mwingine, isipokuwa misikiti mitatu. Ikiwa ataweka nadhiri kufanya hivyo katika al-Masjid al-Haraam, itamlazimu kwake kufanya hivyo. Ikiwa ataweka nadhiri ya kufanya I´tikaaf ndani ya msikiti wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), basi itafaa kwake kufanya I´tikaaf ndani ya al-Masjid al-Haraam. Ikiwa ataweka nadhiri ya kufanya I´tikaaf katika al-Masjid al-Aqswaa´, basi anaweza kuifanya katika msikiti wowote kati ya hiyo miwili anaoutaka.
Inapendekezwa kwa mwenye kufanya I´tikaaf kujishughulisha na kufanya mambo ya kumkurubisha kwa Allaah na kujiepusha na maneno na matendo yasiyomhusu. I´tikaaf haiharibiki kwa lolote kati ya hayo.
Asitoke msikitini isipokuwa kwa jambo ambalo hana budi kulifanya, isipokuwa ikiwa ameweka sharti. Wala hatofanya tendo la ndoa na mwanamke. Itafaa akiwa njiani kuuliza hali ya mgonjwa au mtu mwingine, bila kwenda kwake.
- Muhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy (afk. 620)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: ´Umdat-ul-Fiqh, uk. 43
- Imechapishwa: 04/11/2026
Maana yake ni kulazimiana na msikiti kwa ajili ya kumtii Allaah (Ta´ala) ndani yake. Hiyo ni Sunnah, isipokuwa ikiwa ni nadhiri, basi inawajibika kuitimiza.
Ni sahihi kwa mwanamke kufanya I´tikaaf katika kila msikiti isipokuwa mahali pa kuswalia nyumbani kwake. Si sahihi kwa mwanaume kukaa I´tikaaf isipokuwa ndani ya msikiti ambao kunaswaliwa swalah ya mkusanyiko. I´tikaaf yake katika msikiti ambao kunaswaliwa swalah ya ijumaa ndio bora.
Yule mwenye kuweka nadhiri ya kufanya I´tikaaf au kuswali katika msikiti fulani, basi inaruhusiwa kwake kufanya hivyo katika msikiti mwingine, isipokuwa misikiti mitatu. Ikiwa ataweka nadhiri kufanya hivyo katika al-Masjid al-Haraam, itamlazimu kwake kufanya hivyo. Ikiwa ataweka nadhiri ya kufanya I´tikaaf ndani ya msikiti wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), basi itafaa kwake kufanya I´tikaaf ndani ya al-Masjid al-Haraam. Ikiwa ataweka nadhiri ya kufanya I´tikaaf katika al-Masjid al-Aqswaa´, basi anaweza kuifanya katika msikiti wowote kati ya hiyo miwili anaoutaka.
Inapendekezwa kwa mwenye kufanya I´tikaaf kujishughulisha na kufanya mambo ya kumkurubisha kwa Allaah na kujiepusha na maneno na matendo yasiyomhusu. I´tikaaf haiharibiki kwa lolote kati ya hayo.
Asitoke msikitini isipokuwa kwa jambo ambalo hana budi kulifanya, isipokuwa ikiwa ameweka sharti. Wala hatofanya tendo la ndoa na mwanamke. Itafaa akiwa njiani kuuliza hali ya mgonjwa au mtu mwingine, bila kwenda kwake.
Muhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy (afk. 620)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: ´Umdat-ul-Fiqh, uk. 43
Imechapishwa: 04/11/2026
https://firqatunnajia.com/58-itikaaf/