57. Makatazo ya kufunga na usiku wa makadirio

Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza kufunga siku mbili: siku ya ´Iyd-ul-Fitwr na pia siku ya ´Iyd-ul-Adhwhaa. Amekataza kufunga siku za Tashriyq. Isipokuwa kwamba ametoa ruhusa ya maalum ya kufunga kwa mwenye kufanya Hajj ya Tamattu´ ambaye hakupata mnyama wa kuchinja.

Usiku wa makadirio hupatikana katika siku zenye witiri katika kumi la mwisho la Ramadhaan.

  • Muhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy (afk. 620)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ´Umdat-ul-Fiqh, uk. 42-43
  • Imechapishwa: 04/11/2026