Swawm bora zaidi ni funga ya Daawuud (´alayhis-Salaam); alikuwa akifunga siku moja na akila siku moja[1].
Funga bora zaidi baada ya mwezi wa Ramadhaan ni mwezi wa Allaah ambao wanauita Muharram.
Hakuna siku ambazo matendo mema ndani yake yanapendwa zaidi na Allaah kuliko siku kumi za Dhul-Hijjah.
Mwenye kufunga Ramadhaan na akaifuatisha kwa siku sita za Shawwaal basi ni kana kwamba amefunga mwaka mzima.
Kufunga siku ya ´Aashuuraa´ ni kafara ya mwaka mmoja.
Kufunga siku ya ´Arafah ni kafara ya miaka miwili. Hata hivyo haipendezi kwa aliye ´Arafah kufunga siku hiyo.
Inapendekezwa kufunga siku nyeupe, jumatatu na alkhamisi.
Mwenye kufunga swawm ya kujitolea ndiye mwenye uamuzi juu ya nafsi yake; akitaka hufunga, na akitaka hufungua. Wala halazimiki kulipa. Hukumu ni hiyohiyo katika ´ibaadah nyingine za kujitolea, isipokuwa ´ibaadah ya Hajj na ´Umrah – kwani ni wajibu kuzikamilisha na kulipa kile kilichoharibiwa miongoni mwao.
[1] al-Bukhaariy (1131) na Muslim (1159).
- Muhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy (afk. 620)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: ´Umdat-ul-Fiqh, uk. 42
- Imechapishwa: 04/11/2026
Swawm bora zaidi ni funga ya Daawuud (´alayhis-Salaam); alikuwa akifunga siku moja na akila siku moja[1].
Funga bora zaidi baada ya mwezi wa Ramadhaan ni mwezi wa Allaah ambao wanauita Muharram.
Hakuna siku ambazo matendo mema ndani yake yanapendwa zaidi na Allaah kuliko siku kumi za Dhul-Hijjah.
Mwenye kufunga Ramadhaan na akaifuatisha kwa siku sita za Shawwaal basi ni kana kwamba amefunga mwaka mzima.
Kufunga siku ya ´Aashuuraa´ ni kafara ya mwaka mmoja.
Kufunga siku ya ´Arafah ni kafara ya miaka miwili. Hata hivyo haipendezi kwa aliye ´Arafah kufunga siku hiyo.
Inapendekezwa kufunga siku nyeupe, jumatatu na alkhamisi.
Mwenye kufunga swawm ya kujitolea ndiye mwenye uamuzi juu ya nafsi yake; akitaka hufunga, na akitaka hufungua. Wala halazimiki kulipa. Hukumu ni hiyohiyo katika ´ibaadah nyingine za kujitolea, isipokuwa ´ibaadah ya Hajj na ´Umrah – kwani ni wajibu kuzikamilisha na kulipa kile kilichoharibiwa miongoni mwao.
[1] al-Bukhaariy (1131) na Muslim (1159).
Muhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy (afk. 620)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: ´Umdat-ul-Fiqh, uk. 42
Imechapishwa: 04/11/2026
https://firqatunnajia.com/56-swawm-ya-kujitolea/