Baadhi ya marafiki zetu – Hanaabilah – na wanachuoni wengine wanasema kwenye vitabu vyao kwamba ni sawa kwa yule mwenye kusibiwa kuvaa kitu kichwani mwake kinachojulisha msiba wake. Baadhi ya marafiki zetu Yerusalamu hufunga nywele pasi na kuchukulia kama ada. Hoja yao ni kwamba taazia ni Sunnah na hili linawasahilishia watu zile hali mbalimbali za misiba.

Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amekemea kitendo hichi na kusema:

“Ni jambo lisilokuwa na shaka kwamba Salaf walikuwa hawafanyi hivi. Haikupokelewa kutoka kwa yeyote katika Maswahabah na Taabi´uun.”

Kutakuja mapokezi ya wazi – Allaah akitaka – yanayotilia nguvu maoni haya. Ishaaq bin Raahuyah alikuwa akichukia mtu kuacha anavaa kawaida kama alivyozowea wakati wa msiba na Allaah ndiye anajua zaidi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Muhammad al-Hanbaliy al-Manbajiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tasliyatu Ahl-il-Maswaa-ib, uk. 121
  • Imechapishwa: 27/10/2016