218 – Ibn Kaasib ametuhadithia: ´Abdul-´Aziyz bin Muhammad na Ibn Abiy Haazim wametukhabarisha, kutoka kwa al-´Alaa’ bin ´Abdir-Rahmaan, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Abu Hurayrah, ambaye amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Harakieni kufanya matendo kabla ya kipande cha usiku wenye giza. Mtu atafika asubuhi akiwa ni muumini na ikifika jioni tayari ameshakuwa kafiri, na anafika jioni akiwa ni muumini na ikifika asubuhi tayari ameshakuwa kafiri. Anaiuza dini yake kwa sababu ya dunia.”[1]

219 – Ahmad bin Muhammad bin Nayzak ametukhabarisha: Abu Ahmad ametukhabarisha: Israa’iyl ametukhabarisha, kutoka kwa Abu Yahyaa, kutoka kwa Mujaahid, kutoka kwa Ibn ´Abbaas, ambaye amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Watu watauza dini yao kwa vitu vya kidunia.”[2]

[1] Muslim (186).

[2] at-Twabaraaniy katika “al-Awsatw” (5806). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “as-Swahiyhah” (1267).

  • Muhusika: Imaam Abu Bakr Ahmad bin Abiy ´Aaswim ash-Shaybaaniy (a.f.k. 287)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-uz-Zuhd, uk. 58
  • Imechapishwa: 20/07/2025