142 – Umm Salamah (Radhiya Allaahu ´anhaa), mke wake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), ameeleza kuwa amemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:
“Hakuna mja yeyote anayepatwa na msiba na akasema:
إِنَّا لله وإِنَّا إِلَيْه راجعونَ اللهُمَّ أَجِرْني في مُصِيبَتي وَأَخْلِفْ لي خَيْراً منها
”Hakika sisi ni wa Allaah na Kwake ndiko tutarejea. Ee Allaah! Nilipe kwa msiba wangu na Unipe badala yake kheri kuliko hiyo.”
isipokuwa humlipa kwa msiba wake na humpa badala ilio bora kuliko hiyo.” Wakati Abu Salamah alipofariki, nikasema kama alivyoamrisha Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Na Allaah akanipa ambaye ni mbora kuliko yeye; naye ni Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).”[1]
Ameipokea Muslim.
MAELEZO
Du´aa hii inapendeza wakati wa kupatwa na msiba. Ndani yake imekuja kwamba mwenye kusema du´aa hii basi Allaah atamlipa juu ya msiba wake. Kwa maana nyingine ni kwamba atamlipa ujira na thawabu na aidha atampa kheri kuliko alichopoteza. Ni sharti mtu aiseme hali ya kuyakinisha yale yaliyosemwa na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Umm Salamah (Radhiya Allaahu ´anhaa) aliyasema hali ya kuwa ni mwenye yakini nayo. Ndipo Allaah akampa badala yake Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).
[1] Muslim (918).
- Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 135
- Imechapishwa: 15/11/2025
142 – Umm Salamah (Radhiya Allaahu ´anhaa), mke wake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), ameeleza kuwa amemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:
“Hakuna mja yeyote anayepatwa na msiba na akasema:
إِنَّا لله وإِنَّا إِلَيْه راجعونَ اللهُمَّ أَجِرْني في مُصِيبَتي وَأَخْلِفْ لي خَيْراً منها
”Hakika sisi ni wa Allaah na Kwake ndiko tutarejea. Ee Allaah! Nilipe kwa msiba wangu na Unipe badala yake kheri kuliko hiyo.”
isipokuwa humlipa kwa msiba wake na humpa badala ilio bora kuliko hiyo.” Wakati Abu Salamah alipofariki, nikasema kama alivyoamrisha Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Na Allaah akanipa ambaye ni mbora kuliko yeye; naye ni Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).”[1]
Ameipokea Muslim.
MAELEZO
Du´aa hii inapendeza wakati wa kupatwa na msiba. Ndani yake imekuja kwamba mwenye kusema du´aa hii basi Allaah atamlipa juu ya msiba wake. Kwa maana nyingine ni kwamba atamlipa ujira na thawabu na aidha atampa kheri kuliko alichopoteza. Ni sharti mtu aiseme hali ya kuyakinisha yale yaliyosemwa na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Umm Salamah (Radhiya Allaahu ´anhaa) aliyasema hali ya kuwa ni mwenye yakini nayo. Ndipo Allaah akampa badala yake Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).
[1] Muslim (918).
Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 135
Imechapishwa: 15/11/2025
https://firqatunnajia.com/57-duaa-kwa-mwenye-kupatwa-na-msiba/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket