al-´Ayyaashiy amesema pindi alipokuwa akifasiri Aayah:
إِنَّ أَوْلَى النَّاسِ بِإِبْرَاهِيمَ لَلَّذِينَ اتَّبَعُوهُ وَهَـٰذَا النَّبِيُّ وَالَّذِينَ آمَنُوا ۗ وَاللَّـهُ وَلِيُّ الْمُؤْمِنِينَ
“Hakika watu waliokaribu zaidi kwa Ibraahiym ni wale waliomfuata kama mfano wa huyu Nabii na wale walioamini. Na Allaah ni Mlinzi wa waumini.”[1]
“´Aliy bin an-Nu´maan ameeleza kuwa Abu ´Abdillaah amesema kuhusiana na maneno Yake:

“Hakika watu waliokaribu zaidi kwa Ibraahiym ni wale waliomfuata kama mfano wa huyu Nabii na wale walioamini. Na Allaah ni Mlinzi wa waumini.”[2]
“Bi maana maimamu na wafuasi wao.”[3]
Allaah amemtakasa Abu ´Abdillaah na familia yake kutokamana na uongo huu. Wako wapi Maswahabah watukufu? Iko wapi familia ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika Maswahabah na waliokuja baada yao? Wako wapi waislamu wakweli wa Ummah huu?
Sisi tunasema watu waliokaribu zaidi na mayahudi, waabudu moto na manaswara ni mazanadiki na Baatwiniyyah ambao ni maadui wa Allaah na Mitume na khaswa khaswa Muhammad na Ibraahiym (Swalla Allaahu ´alayhimaa wa sallam):
مَا كَانَ إِبْرَاهِيمُ يَهُودِيًّا وَلَا نَصْرَانِيًّا وَلَـٰكِن كَانَ حَنِيفًا مُّسْلِمًا وَمَا كَانَ مِنَ الْمُشْرِكِينَ
“Ibraahiym hakuwa myahudi wala mnaswara – lakini alikuwa na imani safi na ya asli na muislamu; na hakuwa miongoni mwa washirikna.”[4]
Maswahabah wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na wale wenye kuwafuata ndio waumini wa kweli na ndio wafuasi wa Muhammad na Ibraahim (Swalla Allaahu ´alayhimaa wa sallam).
[1] 03:68
[2] 03:68
[3] Tafsiyr al-´Ayyaashiy (1/177).
[4] 03:67
- Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 92
- Imechapishwa: 03/04/2017

Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 92
Imechapishwa: 03/04/2017
https://firqatunnajia.com/57-al-ayyaashiy-upotoshaji-wake-wa-nne-wa-aal-imraan/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)