14 – Maymiyn bin Mahraan amesema:

”Niliingia kwa Umm-ud-Dardaa´ na nikamuona amevaa shungi nene inayoshuka mpaka kwenye paji lake la uso. Ilikuwa fupi akairefusha kwa mkanda. Sikuwahi kuingia nyumbani kwake wakati wa swalah isipokuwa nilimkuta akiswali.”[1]

[1] Ibn ´Asaakir katika “Taariykh Dimashq” kupitia kwa al-Baghawiy: ´Iysaa bin Saalim ash-Shaashiy ametuhadithia: Abul-Maliyh ametuhadithia, kutoka kwa Maymuun. Cheni yake ya wapokezi ni nzuri. Abul-Maliyh al-Hasan bin ´Umar ar-Raqqiy ni mwenye kuaminika na ni mmoja katika wasimulizi wa “at-Tahdhiyb”. ash-Shaashiy ni mwenye kuaminika kwa mujibu wa Ibn Hibbaan katika “at-Thiqaat” na al-Khatwiyb katika “Taariykh Baghdaad”. 

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Jilbaab-ul-Mar-ah al-Muslimah, uk. 102-103
  • Imechapishwa: 02/10/2023