213 – Abu Bakr ametukhabarisha: Shariyk ametukhabarisha, kutoka kwa ar-Rakiyn, kutoka kwa Nu´aym bin Handhwalah, kutoka kwa ´Ammaar bin Yaasir, kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), ambaye amesema:

“Yeye ambaye ana nyuso mbili duniani, basi siku ya Qiyaamah atakuwa na ndimi mbili za moto.”[1]

214 – al-Maqdamiy ametukhabarisha: Abu Daawuud ametukhabarisha: Shariyk ametukhabarisha, kutoka kwa ar-Rakiyn, kutoka kwa Qabiyswah bin an-Nu´maan (au an-Nu´maan bin Qabiyswah), kutoka kwa ´Ammaar bin Yaasir, kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), ambaye amesema:

“Yeye ambaye ana nyuso mbili duniani, basi atakuwa na ndimi mbili za moto.”[2]

215 – al-Maqdamiy ametukhabarisha mfano wa hiyo: Abu Ahmad ametukhabarisha: Shariyk ametukhabarisha, kutoka kwa ar-Rakiyn, kutoka kwa Nu´aym bin Handhwalah, kutoka kwa ´Ammaar bin Yaasir, kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

216 – Abush-Sha´thaa’ ametukhabarisha: Sulaymaan bin Hayyaan ametukhabarisha, kutoka kwa Ismaa´iyl bin Muslim, kutoka kwa al-Hasan na Qataadah, kutoka kwa Anas bin Maalik, ambaye amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yeyote aliyekuwa na ndimi mbili duniani, basi Allaah (Tabaarak wa Ta’ala) atamjaalia siku ya Qiyaamah kuwa na ndimi mbili za moto.”

217 – Ayyuub al-Wazzaan ametukhabarisha: Marwaan ametuhadithia, kutoka kwa Ismaa´iyl bin Muslim, kutoka kwa al-Hasan, kutoka kwa Anas bin Maalik, ambaye ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yeyote aliyekuwa na ndimi mbili duniani, basi Allaah (Tabaarak wa Ta’ala) atamjaalia siku ya Qiyaamah kuwa na ndimi mbili za moto.”

[1] Abu Daawuud (4873). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh-ul-Jaamiy´” (6496).

[2] Swahiyh kupitia zingine kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb” (2950).

  • Muhusika: Imaam Abu Bakr Ahmad bin Abiy ´Aaswim ash-Shaybaaniy (a.f.k. 287)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-uz-Zuhd, uk. 56-57
  • Imechapishwa: 20/07/2025