Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Ikiwa uombezi wote ni wa Allaah na wala hautokuwa isipokuwa baada ya idhini Yake, na wala hatoombea Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wala mwengine yeyote mpaka Allaah amruhusu – na wala Allaah hatowaidhinishi isipokuwa tu wapwekeshaji – imekubainikia ya kwamba uombezi wote ni wa Allaah pekee. Hivyo mimi naitafuta kutoka Kwake [Allaah]. Ninasema: “Ee Allaah! Usiniharamishie uombezi wake, Ee Allaah! Nakuomba unikubalie uombezi wake kwangu” na mfano wa hayo.

MAELEZO

Hapa mtunzi (Rahimahu Allaah) anachotaka kuonyesha ya kwamba ikiwa uombezi wote ni wa Allaah, na uombezi haupitiki isipokuwa baada ya idhini Yake na kwa yule Anayemridhia – na hawi radhi isipokuwa kwa wapwekeshaji peke yao – basi hilo litalazimisha mtu kutomuomba uombezi yeyote isipokuwa Allaah (Ta´ala) pekee. Kwa msemo mwingine uombezi hauombwi kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ndio maana badala yake mtu anaweza kusema:

“Ee Allaah! Nikubalie uombezi wa Mtume Wako. Ee Allaah! Usininyime uombezi wake” na mfano wa matamshi kama hayo.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-is-Shubuhaat, uk. 69-70
  • Imechapishwa: 24/11/2023